Kumbe na sisi kina baba tuna umuhimu????????

23:15:00 Unknown 0 Comments

Wakati nikiwa mdogo nilifikiri baba alikuwa akinichukia, kila muda alitumia sauti ya kuamuru na yenye ukali wa kuogopesha kila aliponisemesha au kuniambia kitu.

Alitupa sheria za kufuata pale nyumbani, kwa mfano hautakiwi kuigusa radio, kufungua kabati na friji, kwend akwa majirani na kwa kila aliyezivunja sheria zile alipewa adhabu kali sana.

Kila tulipofanya jambo baya,mama yetu alituambia baba akija nitamwambia mmefanya hiki au kile and baba atatuua kwa viboko na adhabu nyinginezo na kilawakati baba aliporudi na mama akamwambia tulipigwa sana.

katika umri wa miaka 7 kushuka nilimchukia sana baba. Nilipoanza kukua alipunguza baadhi ya vikwazo na akaanza kuturuhusu kufanya vitu ambavyo mwanzo alitukataza.

Nilopkuwa na umri wa miaka 15 nikaanza kuonja upendo wake kwangu, na kilanilipoenda shuleni alinipa ada, fedha ya mfukoni kwa ajili ya matumizi yangu shuleni na alitabasamu na kiola niliporudi baada ya shule kufunga alinikaribishwa kwa chakula kizuri sana.

Sasa nina miaka 28 na ananipigia simu na kuniuliza lini nitapata nafasi niende kuwatembelea. Na kila ninapowatembelea najihisi kulia muda wa kuondoka ukifikia.

Funzo

Maelekezo na sheria ambazo baba au wazazi walitupatia lengo kuu ilikuwa ni kutufanya sisi tuwe salama 

baba ana nafasi ya muhimu sana katika maisha ya kila mtoto katika makuzi yake. Mfano jinsi anavyojituma ili ule, uvae, ucheze, usome, utibiwe ukiumwa na kila kitu kizuri utakachokipenda.

Tunavipata vyote kwa mapenzi ya baba na jitihada zake.

Kama umekumbuka kumshukru baba yako leo andika ASANTE BABA kisha share 

USISAHAU KU-LIKE Tabasamu na Fuledi

You Might Also Like

0 comments: