Dogo mbulula kuliko madogo wote

13:38:00 Unknown 0 Comments

Dogo kaingia saluni ya mtaani kwao, kinyozi akamnong'oneza mteja: unamuona huyo dogo anayeingia, ni kilaza na mbulula hakuna mfano. Booonge ya mjinga. Ziro kabisa. Angalia, ngoja nikuhakikishie kwamba dogo ni mpumbavu. Kinyozi akachukua noti ya buku 2 akaweka upande mmoja wa meza na noti ya buku 1 akaweka upande mwingine. Akamuita dogo akamwambia unataka ipi kati ya hizo noti mbili? Dogo akanyonya kidole, akachukua noti ya buku 1 akaondoka zake. 

Kinyozi akamwambia yule mteja, umeona? Mara zote dogo ndo hivyo hivyo. Hajifunzi kabisa ipi kubwa ipi ndogo. Kilaza. 

Baadaye yule mteja akaondoka saluni, mtaani akakutana na yule dogo analamba booonge la ice cream, akamuuliza: hivi kwa nini ulichukua noti ya buku ukaacha ya buku mbili? Dogo akamjibu: siku nikichukua noti kubwa, yule kinyozi atajua nimeanza kuwa na akili na mchezo wa kufaidi hela utaishi. Muache aendelee kuniona mbulula nifanye yangu.

You Might Also Like

0 comments: