Mungu anapoamua kusema kitu
Mwanamke mmoja masikini
sana alipiga simu katika kipindi kimoja maarufu kilichokuwa kikirushwa na radio
moja ya dini na kusema alikuwa anahitaji msaada ili apate chakula cha familia
yake kwa siku hiyo.
Tajiri mmoja mwenye
dharau na asiyependa kuona MUNGU akitukuzwa huku akiwa anasikiliza kile kipindi
akaamua afanye kitu kwa huyu mama.
Akainakili anuani ya yule
mama na kisha akampa secretary wake fedha na kuwatuma waende sokoni na kununua
vitu vingi pamoja na vyakula na fedha nyingi za kumpa yule mama masikini na akasema akiwauliza nani kaleta nyie semeni
mmetumwa na shetani wa kibongo.
Baada ya kununua na
kubaki na fedha kama alivyoelekezwa na tajiri, yule secretary akafika kwa yule
mama na akashusha mizigo na kumpa zile fedha pia kama alivyoambiwa.
Yule mama akaipokea ile mizigo kwa furaha
na kuwashukuru na kuanza kuingiza mizigo ile ndani. Secretary akamuuliza yule
mama, “Je ulitaka kujua nani katutuma tuilete hii mizigo?”
Yule mama akasema, “HAPANA,
Haijalishi nani kaniletea mizigo hii baada ya kusikia nikiomba kwa kupiga ile
simu pale radioni, Maana MUNGU akiagiza hata shetani hufanya kama MUNGU
alivyoagiza”
Unajifunza nini
Mafanikio yako ni kwa
sababu ya uwepo wa nguvu za MUNGU, Hivyo Mungu daima atamalizia mipango yako na
kukupa mafanikio endapo utazidi kumcha yeye na kumshirikisha katika kila kitu,
haitajalisha ugumu wa jambo hilo kwa mungu kila kitu chawezekana.
Mungu atakupeleka mpaka juu ya kilele cha mafanikio na kukufungulia kitabu cha kumbukumbu ya mapito yako nasi tutajifunza kutoka kwa mafanikio yako.
Kwa sababu wewe uko nafasi ijayo kupata mafanikio mazuri kwa uweza wa “MUNGU”
0 comments: