Sitaisahau siku hii ambayo kidogo nimpoteze mama yangu kwa tama za utajiri wa mkato
Maisha yalizidi kuwa magumu na sikuwa na jinsi zaidi ya
kusafiri kutoka Moshi na kwenda kusini mwa tanzania kusaka maisha.
Tangu mzee afariki maisha yalikuwa magumu kwetu na kama
ujuavyo maisha ya mama zetu wa kiafrika, baba zetu waliwasahau katika kuwaweka karibu na utafutaji wa fedha
wao walibaki nyumbani sasa fikiri mzee kafariki na tuko watoto sita tutaishije?
Mama yangu nilimwahidi lazima kabla ya uzee wake au kifo
kumchukua lazima afurahie matunda yake kupitia mimi na alikuwa na furaha kila siku kusia maneno hayo toka kwangu.
Nilifika mkoa huo kusini mwa Tanzania na nilishangazwa kuona
mtoto mdogo kuliko mimi ana utajiri wa kutisha.... duuuh mate yalikuwa
yakinidondoka hasa ukizingatia sikuwa na kipato cha kuanza biashara yangu wala elimu kubwa ikabidi yule kijana aniajiri katika shamba lake la chai na mimi nikawa msimamizi pale.
Baada ya mwaka mmoja wa kuzoea pale huku nikifanikiwa kupata
hela kidogo na kumtumia mama yangu niaanza kuona mambo sio mabaya sana ila nakumbuka kuna jamaa yangu mmoja aliyekuja nyuma yangu
ghafla nikaanza kusikia kuwa jamaa kashapata utajiri maana mara ananunua viwanja
anajenga hotel na fedha kibao. Ndipo nikaambiwa kuwa mimi tuu ndio fala wenzangu wote huenda kijiji jirani ambako kuna mzee mmoja ambaye yeye huwapa vijana utajiri.
Kwa siri nikajiandaa na nikamtembelea yule mganga na
hakuniambia nimpe hela alisema ananipa dawa nikishapata fedha niende
kumshukuru. Ila akasema nilale pale kwani kuna mtihani nitaufanya kabla ya
kwenda kuitumia ile dawa na kuniuliza kama sio mwoga na nipo jasiri.
Jioni ile alinipa mkuki na kuniambia nipite uchochoro mmoja
na kuwa nitakutana na kitu cha kutisha nisikiogope na nikienda hatua chache
nitakutana na cha pili wala nisiogope pia ila cha tatu tu kikitokea niurushe mmkuki
na kukiua pale pale kisha nirudi haraka kwa mganga.
Nikauchukua mkuki na
kuanza kuufuta ule uchochoro, hatua chache tuu nikaona bonge la nyoka likinijia kwa mbele nikajikaza nae akasepa zake wakati huo mkojo na jasho
ninaninyanyasa, hatua chache mbele akatokea simba wa ajabu nae ananifuata
nikajikaza akapita na kupotea ile najiandaa kuuweka mkuki sawa ili kile cha
tatu nikipe mkuki mara naona mama yangu ndio anakuja, niliutupa mkuki na kwenda
kwa mganga na kumwambia aisee nimeshindwa mimi plz nipe jaribio jingine hili la
mama sio.
Mganga akachukia na kunipa ndoano pamoja na fimbo yake na kusema nenda hapo mtoni
iinginze hii kwenye maji kitu ukihiisi kama samaki kimenasa wewe ibebe ndoano na
bila kuangalia nileteee.
Nikafanya hivyo na ile ndoano ilivyokuwa nzito
nikainyanyua na kuiweka mgongoni na kisha kuondoka ila kabla sijafika kwa
mganga nikasema ngoja nigeuke na kuangalia ni nini, duuuh kumbe tena nimemvua
mama yangu.
Nikakimbia na kumwambia mganga mie nimeshindwa huku nikiwa nimechanganyikiwa akanipa dawa na kusema kimbia sana tafuta
usafiri uanze kwenda moshi ukifika pale mmwagie mama yako maji haya.kwani muda
huu atakuwa kaanguka na wamemkimbiza hospitali maana utajiri huu ni lazima mama
yako au ndugu afe ili upate.
Niliunga unga usafiri na siku ya pili jioni nikawa moshi, kweli wakaniambia mama alianguka tu jana jioni na hawajui kuna nini,
nikamwamgia dawa ile akapona na ndio nikawasimulia kilichotokea.
Wakanisema sana sana na sasa nimeokoka na nimepata utajiri kwa njia ya halali na ninakoma na
nimekoma kuupenda utajiri wa mkato…………….
Sitaisahau siku hii ambayo kidogo nimpoteze mama yangu kwa tama
za utajiri wa mkato
0 comments: