Rafiki wa facebook aniwekea kisu shingoni mida hii

18:58:00 Unknown 0 Comments

Leo asubuhi nimeingia kazini mapema sana kuliko
kawaida yangu baada ya kugombana na wife
home.

Nilipofika nikatulia kwenye computer na kuwa
busy na mitandao ya kijamii kujipa nafasi ya
kusahau maugomvi.
Ile kufungua facebook tu nikakutana na friend
request ya binti mmoja mtamu sana mwenye pic
za kuvutia na kuanza kuchati naye.
Kwa kweli binti yule anajua sana kuchati na
huwezi amini mpaka kufikia mida ya saa nne
nilikuwa sijafanya kazi yoyote pale ofisini kwa
utamu wa text zake.

Tukazidi kufahamishana na yeye akadai ana mme
anaye pendana naye sana na mimi nikawa
namwambia nina mke ila ana longo longo sana
hivyo simpendi kiviiile ni basi tu yaani.

Tukaendelea kuchati na akawa anaonekana
anasogea sogea kwangu na akaniuliza niwe
muwazi kumwambia kama tangu nuanze ndoa
kuna wanawake nimewahi tembea nao ndio
anikubali kuwa nae kwani anaogopa magonjwa,
nikampa idadi yake bila kusita na hata
alivyoomba majina yao nikampa yale ya mwanzo
tu.

Akanipenda sana kwa kuwa muwazi na kuniambia
atafikiria kwa kuwa mimi ni mkweli sana.
Baadae nikamwomba afanye tuonane akanipa
namba ya voda nami baada ya kufurahi
nikamwambia ningempigia jioni hii.
Jioni hii nimeipiga ile namba sauti ni ya mke
wangu na nilipojaribu kumtumia fedha kwa
mpesa, nimeishiwa nguvu kuona ni jina la mke
wangu na hakuwa na laini ya voda kabla.

Jamani nimetoka kazini nipo hapa bar nakunywa
na sijui leo nyumbani itakuwaje kwani hapa
kati nimekuwa mkorofi sana kwa mke wangu na
akasema kuna siku atanibamba tuu.....

Naumia zaidi ile kutoa list ya mabinti niliotembea
nao wote....

You Might Also Like

0 comments: