Kamwe sitaisahau siku mengi aliponipa utajiri,
Ile simu asubuhi ile ilinichanganya kabisa na kunitoa katika usingizi wangu.Hebu fikiri mzee MENGI anakuambia ameipenda idea yako na uende ofisini kwake ukaongee nae na akupe fedha?
Kwangu ilikuwa ni ndoto ya usiku wa manane.
Baada ya simu ile niliamka asubuhi sana na kupanda ndege ya kwenda dar kutoka mbeya.
Sitaki kuongelea experience ya kwanza kupanda ndege ila nakumbuka dar tulifika salama.
Mzee mengi alinipokea ofisini kwake na kweli ni mzee wa busara sana na akaniambia anapenda vijana wa kitanzania ambao huwa wanapenda kufikiri mambo makubwaa.
Nakumbuka nami nikamwambia juu ya changamoto za sekta ya sanaa tanzania na kwa nini nimeamua kuja na idea ya website ambayo itauza miziki , jokes na film za kibongo na wasanii kupata fedha.
Akaikubali sana na kuniambia tutaianza mapema sana. Na naikumbuka ile ofisi yake ni nzuri sana sana.
Wakati naendelea kumpa idea nyingine ambayo aliipenda zaaidi ya ile ya mwanzo mara simu yangu ikawa inaita kwa uaumbufu sana nami nikawa na izima.
Usumbufu ukazidi mpaka nikaamua kuipokea na kuitikia kwa hasira kuwa, "bwana niache nitakupigia nipo kikaoni na mheshimiwa mengi."
Nikashangazwa baada ya yeye kuniitikia na kusema mengi yupi bwana acha kuota wahi stendi ukapande gari na kuwahi safari ya kurudi mbeya.
Niliumia sana na naendelea kuumia kwa kuwa ulikuwa ndoto ya mahela kibao
0 comments: