Safari ya mbeya imenipa majanga..... nyumbani hapakaliki

22:03:00 Unknown 0 Comments



Leo asubuhi nilikuwa nasafiri toka Dar kuelekea Mbeya.. Nikajivuta zangu mpaka kituoni na baada ya basi kuja nikaingia na kwa bahati nzuri nikajikuta nakaa siti moja na bonge la mrembo.

Basi kama ujuavyo sie wanaume ni lazima uanze kumtengenezea Mazingira ili asikuone kuwa wewe ni wakuja au mshamba Fulani hivi.

Nikamsalimia na kisha nikajisachi mfukoni na kuchukua simu yangu nikaanza kusoma post za tabasamu na fuledi baada ya kuridhika nikaiweka mfukoni na kuhukua novel yangu na kuanza kuisoma.

Kufika mitaa ya morogoro nikaona isiwe taabu nikaanza kumpa maneno ya hapa na pale na nikaona mtoto anaanza kuingia laini na akaniambia kuwa yeye sio mwenyeji wa Mbeya ila anaenda kumsalimia rafiki yake kipenzi walieachana nae long time na baada ya kusikia yuko Mbeya na kupata mawasailiano yake akaona aende kumsalimia kabla ya kurudi kumalizia masomo yake huko majuu.

Akaniuliza kama nina familia, nami kwa haraka nikamwambia sina kabisa familia na sasa nafikiri baada ya kumwona yeye naanza kufikiria kuwa na familia…….

Safari ikawa taamu mtoto akaanza kujiachia yaani kuwa huru kabisa na nikawa sasa niko na mke mtarajiwa, mara anilalie mara story za dear zikaanza amini usiamini nikaona ni zaidi ya zali la mentali... yaani mtoto mtamu kama yuyle kunikubali kirahisi vile??? sio jambo la kitoto ati

Tulipoingia Mbeya mie nikamwambia basi kesho tuonane maana mie nashuka kituo ha kwanza kabla ya kufika stand ili niweze pata moja baridi moja ya moto, basi ikatubidi tukabadilishane namba za simu na kuachana huku tukikubaliana tuonane siku ya pili yake ambayo ni kesho ili anipe upako kidogo..he he he raha sana.

Nikashuka zangu na kuendelea na taratibu nyingine iza kula bata huku roho saafi kwani kesho mwanaume mambo yatakuwa mwake mwake…..

Mida hii narudi zangu nyumbani nashangaa kuona yule dada yuko home yaani kaja home na kumbe mke wangu ndio rafiki yake ambaye amekuja kumcheki hapa Mbeya…….

Nimewasalimia na kumchukua mtoto wangu nakuzuga kucheza nae na sasa nipo chumbani jasho lanitoka na sijui nifanyaje...

Yaani sijui yule dada ananionaje na je hawezi kumwambia wife????
Maana nimechanganya mambo hapa.....

You Might Also Like

0 comments: