Ua aina ya rose na kadi vyazua balaa na kunibadilisha mtazamo wangu kabisa

18:29:00 Unknown 0 Comments



Kijana mmoja ambaye alikuwa kaanza kuyapatia maisha yake huko mjini siku moja asubuhi baada ya mama yake kumpigia simu na kumlaumu kwa kuwa kimya mno bila hata ya mawasiliano kwa muda mrefu sana, aliamua kwenda katika duka la kuuzia maua na kadi ili akamtumie mama yake kupitia basi kuondoa ugomvi.

Wakati anashuka pale kwenye gari akamwona mtoto mdogo wa miaka nane hivi akakiwa kakaa pale chini analia kwa uchungu.

Kijana akamsogelea na kumwambia unalia nini? Yule mtoto akajibu, "Nilitaka kumnunulia mama ua la rose na kadi nimekosa kwa kuwa nina 500 tuu na ua pamoja na kadi niitakayo ni 5,000.

Kiajana akacheka na kusema usilie haya twende nikakununulie. baada ya kununua na yeye kununua mahitaji aliyoyataka akamwambia yule mtoto apande gari ili ampeleke nyumbani kwao.

Wakapitia kituo cha basi yule kijana akatuma mizigo iende kwa mama yake na kisha kumchukua mtoto na kumpeleka mpaka kwao.

Yule mtoto aliposhuka akamwambia yule kijana kuwa mama yuko huku twende kijana akamfuata na wakazunguka nyuma ya nyumba na kwenda mpaka kwenye kaburi la mama yake na kisha yule mtoto akasali na kuweka ua na kadi ile.

Kijana alipatwa na mshangao kwa tukio lile alipotoka pale moja kwa moja alienda mpaka kituo kile cha basi na kuichukua ile mizigo aliyoituma kisha akapitia bank na kuchukua fedha ya mafuta na kuendesha gari umbali wa kilomota 700 na kwenda kumkabidhi mama yake zawadi zile na kumwomba msamaha kwa kutokuwa na mawasiliano ya kadibu.

Hebu jiulize

Ni mara ngapi umewakumbuka wazazi wako na kuwatumia zawadi katika mwaka huu?

Ni mara ngapi wazazi au walezi wamekulaumu kwa kuwa busy bila kuwajali?

Na ni mara ngapi umetumia hata muda wa kazi kuchati na wapenzi wapya au kuwapigia simu bila kusingizia uwingi wa kazi zako????

Funzo

Anza sasa kuwapenda wazazi wako kwani kuna watu wanatamani wangepata bahati ya kuwa na wazazi wao muda huu na kuwajali.

Kazi za kidunia zipo lakini pia wazazi wana nafasi kubwa sana na wanahitaji ukaribu wako kwao

Mtoto huyu amenikumbusha leo mimi kumpigia simu mama na kumsalimia baada ya kutofanya hivyo kwa wiki kadhaa

Umejifunza kitu?

Usisahau kualika rafiki yako katika ukurasa huu Tabasamu na Fuledi

You Might Also Like

0 comments: