usisome haikuhusu

16:23:00 Unknown 0 Comments

Nilifika asubuhi ile na kushuhudia duka langu likiwa limevunjwa na hakuna hata chembe ya kitu chochote cha thamani kilichobakia mle ndani.

Nilihisi kuchanganyikiwa kwani nikaanza kufikiri jinsi nitavyoanza kukimbizana na bank kurudisha fedha na kama haitoshi kuna mzigo niliuchukua na sikuwa nimeulipia hata senti tano na tisa kumi ni jinsi gani nitaweza sasa kuiendesha familia yangu.

Ilinilazimu niende kwanza home nikajipumzishe kwanza kabla ya kuanza kumsimulia mke wangu. Nakumbuka mara baada ya kuamka na kumsimulia mke wangu hakuisha kulia kwa uchungu wa hali ya juu.

Mwezi mmoja ukapita na kabisa nikawa nimeishiwa hela kwani ile chache iliyokuwa benki ilibidi nianze kupunguzz madeni kabla ya muda kunitupa mkono na deni kuwa kubwa sana.

siku moja jioni nikiwa nimetoka matembezini nikafika nyumbani na kuona kuna ugeni wa watu wanne ambao walifika pale nyumbani kujisitiri baada ya kukosa nyumba ya kulalawageni na walikuwa wakitakiwa kukaa pale kwa mwezi mmoja.








Niliwakaribisha kwa furaha kwani mke alishawakaribisha na walipata kusoma wote enzi hizo na mmoja wao ni wa kijijini kwetu.

Nakumbuka sikulala usiku ule nikiweaza na je nitawezaje kuwatunza pale hyumbani, kamaujuavyo taratibu zetu za kiafrika huwezi mwambia mgeni sasa sina hela nenda tu hotelini, kwanza utaonekana mtu wa ajabu sana.

Siwezi kuongea mwezi ule niliishije ila nalo kumbuka ni kuwa sikuonyesha hata dalili ya kuumia au kulaumu ujio wao, walikula walikunywa na kufurahia na hata wakati wanaondoka walipotaka kuchangia fedha nilikataa kwa moyo mmoja mimi na mke wangu. Mke wangu alifurahi na kuniambia anajua sina hela niliwezaje kuleta yale mahitaji. Nakumbuka nikamwambia nilimwomba sana MUNGU na kila rafiki niliyekuwa nikimwambia anipoe hela alinipa bila shingo upande.

Baada ya wale wageni kuondoka nilianza kuishuhudia miujiza ya ya ajabu katika Maisha yangu, kwanza nilipigiwa simu kutoka kituo kimoja cha polisi na kuambiwa mizigo yangu imekamatwa na iko pale ile iliyoibiwa na baada ya kwenda pale niliipata yote pamoja na gharama zangu za usumbufu kwangu ilikuwa ni kama miujiza.

Wiki moja baadae nilipata tenda ya kugawa vyakula kwenye hoteli mbili kubwa za kufahari na kila wiki tangu pale ilikuwa ni ya Baraka sana kwangu na familia yangu.

Nilichojifunza

Nilipofika dukani siku ile na kushuhudia wale wezi wakiwa wameiba jambo la kwanza nilimwambia MUNGU naomba utende miujiza name niushuhudie ukuu wako na kweli mpaka sasa naushuhudia ukuu wake.

Wale wageni walipokuja niliwafurahia na pia pamoja na hali iliyokuwa ikinikabili jambo la kwanza lilikuwa ni kumwomba MUNGU anipe nujasiri na yeye awalishe wale wageni na kweli mpaka leo siwezi kusimulia mambo yaliendaje ila Nimejifunza kitu.

Mkono ule utoao ndio utakao pokea… wakati nawasaidia wale wageni sikujua wala kutambua kama huko mbeleni ningeweza kuja kupata Baraka kama hizi ila hakuna kisichoshindikana MUNGU akisimamia jambo.

Hebu jiulize

NI mara ngapi unamtegemea MUNGU katika kila jambo lako?

Ni mara ngapi unachukizwa na ujio wa wageni wajapo kwako wakati wewe huna kitu mfukoni????

AMini na mtangulize MUNGU katika kila jambo na utashuhudia miujiza yake katika Maisha yako…..

RUKSA: kusema AMEN pamoja na kushare kama unamtanguliza MUNGU katika Maisha yako.

You Might Also Like

0 comments: