Wangapi wanataka kwenda mbinguni?"
Siku moja mwalimu wa dini alikuwa anafundisha wanafunzi wa darasa la 1,akauliza,"Wangapi wanataka kwenda mbinguni?"Darasa zima wakanyosha mikono,kasoro mwanafunzi mmoja tu!
Mwalimu akamuuliza,"Wewe hutaki kwenda mbinguni?"
Dogo akajibu hataki.
Mwalimu akamuuliza,"kwanini."
Dogo akajibu,"Mama ameniambia nikitoka shule nisipite popote! Niende moja kwa moja nyumbani!!"
0 comments: