Mtoto wa kike wa miaka 15 amfanya mama azimie
Mama mmoja aliingia chumba cha mtoto wake wa kike na kushangazwa kuona kitanda kimetandikwa vizuri na mtoto wake pamoja na baadhi ya mabegi yake yametoweka.
Mezani akaona bahasha moja nzuri na kufungua ndani akaona kuna barua ikambidi afungue na kuanza kuisoma huku kaka pale kitandani.
Barua iliandikwa hivi:
Mama yangu mpenzi,
Kwanza naomba uamini ya kuwa nimeandika barua hii nikiwa na huzuni na maumivu moyoni hasa nikikufikiria wewe.
Nimeamua kuondoka nyumbani na niko kwa mpenzi wangu Fuledi nimeamua kufanya hivyo ili kuepuka ugomvi ambao ungezuka kati yangu wewe na baba.
Nimekuwa nikiwa na Fuledi kwa muda na ni mtu mwenye roho nzuri sana. Na sio roho nzuri tuu lakini pia muonekano wake hata kama ana tattoo nyingi, ndevu , makovu mwilini, ulevi, matumizi ya madawa ya kulenya pamoja na mke aliyemtelekeza huko kijijini, lakini kwa upande wangu nimempenda na kikubwa ni hii mimba niliyonayo naamini nitajifungua na kuishi salama na yeye.
Yeye ni dereva wa malori yaendayo Congo na watu humzushia kuwa ameathirika na kwamba eti kila kituo yeye ana tembea na wanawake wanaojiuza ila mimi naamini ni majungu maana usiamini maneno ya watu ukishakuwa kwenye ndo.
Kwa sasa hana nyumba maalamu ila tunaweza kulala kwa muda kwenye lori lake moja na anataka tuwe na watoto wengi jambo ambalo limekuwa ndoto yangu pia mama,hebu fikiria unakuwa na wajukuu wengi kutoka kwangu? Naamini utafurahi sana mama.
Pia jambo zuri ni kwamba Fuledi kanifundisha kuvuta bangi na kasema haina madhara kabisa wala haiumizi na ni dawa hivyo tunafikiria kuanza kupada kwa wingi na kuuza kujipatia fedha kwani sitakuwa na kazi nyingi sasa hivyo bado naendelea kumsikiliza mwalimu wangu.
Chonde chonde mama kumbuka kumwombea sana mme wangu maana ameshaumwa TB mara tano na amedhohofu kidogo hivi karibuni ili aweze kupona na kuendelea kuwa baba wa familia yangu na mkweo pia.
Usiwaze sana mama nina mika 15 tuu ila sasa naweza kujitegemea na pia nazidi pata mafunzo kutoka kwa mme wangu kipenzi na kuna siku nitakuletea mjukuu wako aje ukmsalimia.
Mtoto wako kipenzi,
Shamira.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
NB: Mama hayo hapo juu hayana ukweli wowote niko kwa rafiki yangu matokeo ya mtihani yametoka nimefeli somo moja nimejificha mpaka hasira zako zikipungua ndio nije. Matokeo yako kwenye droo ya viatu mama.
Nilitaka pia ujue pamoja na kufeli huo mtihani nina kipaji cha kuandika hadithi.
Utanipigia hasira za wewe na baba zikipungua ili nije
Nakupenda mama
Tafadhali naomba nipe maoni yako kwa kubofya HAPA
0 comments: