Binti aliyepata mtihani mgumu wa kumchagua mme sahihi wa kuishi nae
Walikuja vijana watatu na kutaka kumposa binti mmoja...
Kijana mmoja alikuwa Tajiri sana..
Kijana wa pili alikuwa Handsome sana...
Kijana wa tatu alikuwa maskini sana..
Baba wa msichana akamwambia bintie,
Mwanangu sikia ushauri wangu kwako,
"Huyu kijana tajiri atakutajirisha sana..
Kijana Handsome utazaa nawe watoto wazuri sana...
Kijana maskini atakufanya uwe maskini sana, sasa uamuzi ni wako..."
Binti akasema, "Baba yangu huyu kijana tajiri hatatosheka na mimi ataowa mke wa pili na watatu na wanne..
Huyu kijana Handsome atapendwa na wanawake wengi kwa uzuri wake..
Na huyu kijana maskini ataishi na mimi peke yangu hatafikiria mwanamke mwingine kwa sababu ya hali yake..."
Hivyo baba nimemchagua huyu kijana maskini,kwani ni maskini wa mali lakini tajiri wa mapenzi na uaminifu...
Rafiki wa Fuledi nawe nakuombea Mungu akupe hekima na busara katika kila ulifanyalo
Changia mawazo yako HAPA
0 comments: