Nifanyeje kumrudisha mpenzi niliye gombana nae?

00:53:00 Unknown 0 Comments


Mimi ni msichana wa miaka 20 na nilikuwa na mpenzi ambaye tulipendana sana ila tuliachana miaka miwili iliyopita.

Kwa kweli kuachana kwetu kulikuwa ni kwa kukoseana, yaani yeye alinikosea nami pia nilimkosea hivyo tulikoseana.

Nilimpenda sana yule mkaka na hadi kesho ntazidi kumpenda na ninatamani sana niwe nae kwa mara nyingine ila sijui nitumie njia gani kumfanya arudi kwangu.

Kumpata mwanaume mwingine naweza coz najiamin mi ni mzuri na sifa ninazo ila moyo wangu wote upo kwake na hata nikiolewa kwa ku-force hahisi hiyo ndoa haitakuwa ndoa.

 Namba zake za simu ninazo na huwa tunawasiliana mara moja moja na kutumiana msg, cha ajabu haoneshi hata dalili ya kutaka kurudi  kwangu.

Naumia sana coz nampenda sana tena sana ila nashindwa nifanye nini ili tuwe pamoja na tufunge pingu za maisha.

Rafiki zangu najua mlio wengi mnajua maumivu ya mapenz hivyo basi nahitaji ushauri toka kwenu. Kama mtanitukana poa ila jua leo kwangu kesho kwako.

Natanguliza shukuran kwa yule atakae toa ushauri wa busara na si matusi

Asante

Toa ushauri wako kwa kubofya hapa

You Might Also Like

0 comments: