Kwa wanaume:
Kuwa na wanawake wengi au vimada kibao hakukufanyi kuwa mwanaume bora, Ila unatakiwa kujionyesha kuwa wewe ni mwanaume mkamilifu kwa kuwa na mpenzi mmoja na kumpa mahaba ya dhati na kumfanya ajione wa pekee katika dunia hii.
Na je kumdanganya binti/mabinti ili ufanye nao mapenzi inakufanya kuwa zaidi ya mwanaume??
Hapana, inakuonyesha jinsi ulivyo kiumbe wa ajabu kwa kutumia mbinu chafu kupata kile unachokitaka.
Hivyo, kama wewe ni mwanaume wa ukweli, unatakiwa kujifunza kuendelea kuwa na mpenzi mmoja ambaye umejitoa kwake kwa moyo wako na akili zako huku ukimpa kila atakacho kadri uwezavyo na kubakia mwaminifu kwake.
Kumbuka, kila unachomfanyia mwanamke kinaonyesha mara mbili yake jinsi wewe ulivyo
0 comments: