Nimeshaharibu tena sijui nifanye nini??? Wadau saidieni kuokoa jahazi
Nilisimuliwa sana na kusoma katika magazeti ya burudani kama vile Tabasamu, Sani na mengineyo juu ya warembo waliopata kutokea hapa duniani na kutikisa miji Fulani Fulani. Na katika majalada yao waliwachona kwa ufasaha baadhi ya mabinti ambao kwa urefu wao, shepu zao na hata nyuso na vifua vyao viliashiria utofauti wao katika jamii.
Nilitamani na kila siku niliomba japo nimpate mmoja na kama haitoshi niweze kuwa nao na nione ufahari wa kuishi duniani na pia nionekane mwanaume wa kweli mbele ya mabinti wengine na hata mbele ya wanaume wenzangu waniogope na kunipa sifa kemkem.
Niliuliza maswali mengi kuwa watu hawa wanapatikana watu, wengi wakasema ukitaka kuona nenda posta dare s salaam na uone watu walivyoumbika au nenda Arusha kawaone wambulu na waairaq nikiwa natafakari hilo nikasoma kitabu kimoja kikaonyesha kuwasifia sana wahabeshi waishio Ethiopia na pia wanyarwandwa kwa Africa na kwa America wakasema kuna brazil na puote rico.
Nikajisemesha mwenye kuwa kazi ipo huko kuwingine sitaenda ila nikaenda posta kweli nilikutana na mabinti wa kutisha ila mbaya zaidi sikuona wakunifaa nikaishia hapo na juhudi zangu za kumpata huyo binti mlimbwende.
Siku moja nikiwa nasafiri kutoka kahama kwenda mwanza nilibahatika kukutana na dada mmoja mbaye nilishindwa kujizuia na kumsalimia ingawa alionekana kaka na baunsa mmoja nikaogopa kupata kilema cha ukubwani kwa kushushiwa kipondo kwa hiyo nikaishia salamu tu.
Miezi michache baadae nikatembelea mkoa mmoja hukoo kaskazini kikazi lakini kwa kuwa safari ilikuwa ya ghafla nikaamua kuondoka bila kuwa na nguo za ziada. Nikafika huko na kuamua kuzingukia katika maboutique mbalimbali kabla ya kuja katika boutique moja lna kuonana na Yule binti tuliyeonana nae tukitoka kahama.
Binti huyu alikuwa mrefu wa kawaida, ana mwonekano wa kuvutia, ana nywele ndefu za asili, amebarikiwa maeneo yote wa sio zao la mchina kama dada zetu wa sasa na zuri kuliko zote ana rangi asilia ambayo kila mtu anaipenda maanisha rangi halisi ya kiafrika.
Nikaduwaa na kwa upole kama nimezinduka baada ya kula kofi la uso nikamwambia dada unanikumbuka? Akaniambia hapana, nikamkumbusha na kutaniana kidogo kuhusu Yule baunsa akacheka na kusema hofu yako tu mie sina mme Yule kaka yangu na tulitoka kmsalimia mama kwa hiyo yeye yupo kwake huko Dar.
Baada ya story zile nikachukua mahitaji yake na namba zake na kisha kuondoka kwenda huko kwenye kazi zangu. Wiki mbili nilizokaa pale juhudi za kumshawishi binti Yule awe wangu zilishindikana pamoja na mitoko ya hapa na pale lakini alikuwa mgumu mithili ya kisiki cha mpingo.
Nikarudi zangu mkoani kwangu na kuendelea kuwasiliana nae bila ya mafanikio nikafika kipindi kidogo niache kuwasiliana lakini roho ikawa inauma.Miezi ikasonga na mawasiliano yakaendelea name nikawa nimekubali hali hiyo na kuwa kama dada na kaka tukisaidiana kwa kila jambo kama vile fedha, mawazo na kila jambo lililohitaji kushauriana kimaisha.
Siku moja majira ya saa kumi nikiwa nyumbani kwangu alinipigia simu na kuniambia, mambo vipi Fuledi, uko mbeya au umesafiri? Nikamwambia sijasafiri nipo tu hapa mbeya si wajua kazi zangu nafanyia nyumbani? Akaniambia naomba unisaidie jambo moja, nikamwambia wewe tu haina shaka kama lipo ndani ya uwezo wangu.

Akaniomba kuwa kuna mdogo wake kaja na kafikia hoteli moja maarufu hapa jijini mbeya ( siitaji maana walininyima tangazo) sasa alitaka nimchukue na kumzungusha mjini kuna mambo anataka kuyaweka sawa kwani siku ya pili ana jambo la muhimu.
Nikamkubalia na akanipa namba ya huyo binti,
Nikawasha gari na kwenda mpaka hoteli hiyo na nilipofika reception nikamtumia text kuwa mimi nimetumwa na dada yako aitwaye bingile kuwa nikusaidie sasa nimefika nipo mapokezi. Akasema poa kisha akapiga simu pale mapokezi na kunichukua mpaka mlango wa chumba hicho.
Kufungua mlango sikuamini macho yangu, Mtoto alikuwa ananizingua hakuna cha mdogo wake wala nini kumbe ni yeye kasafiri na kuja mpaka mbeya, na chumba kile alikipamba kwa maua mekundu, kadi za mapenzi na kiukweli kilikaa kimahaba sana na hakusema neon zaidi ya “FULEDI UTAKUBALI KUWA VALENTINE WANGU?’
Sikujibu nikamrukia ile anataka kunidaka kikashtushwa na maumivu ya uso baada ya kuigonga sakafu .
Kumbe viroba vilinijaa kichwani na muda wote huo nililala bar baada ya kupakia viroba vya konyagi.
Nikanyanyuka huku wahudumu na baadhi ya wanywaji wakinicheka kuichukua boda boda nikiendelea kuwaza ndoto hii na jinsi ya kumpata mrembo huyo..
0 comments: