Kuwa blogger na admin wa baadhi ya page hapa facebook nimejifunza mambo mengi ya msingi katika maisha.

12:52:00 Unknown 0 Comments




1. Unapoandika story ukaiweka kwenye page na isipate watu wengi hukufanya ujihisi kuwa kuna sehemu ilitakiwa uboreshe kazi yako na kuwafanya wengi wawe wamegusika.

Hivyo story ya pili huongeza ubunifu zaidi na kutulia na kisha ikapendwa na watu wengi zaidi na ukapata watembeleaji wengi ambao wataacha mawazo yao.

Hii inanifundisha kuwa hata maisha yanahitaji kuwa na ubunifu na kutokata tamaa zaidi ya kujaribu tena na tena.

2. Kuna watu wao mwanzo wanakuwa ni watu wa kukukatisha tamaa kusema unaandika ujinga au hata kuonyesha hawapendi kile unachokifanya nawe ukajikaza na kuendelea na kila ukiposti wao wakakosoa au hata kupinga sio kwa hoja bali kwa kutopenda tuu kile kinachotoka kwako.

Lakini mwishoni wengi hugeuka na kuwa ndio washabiki wa kazi zako namba moja na hata wengine hawataonyesha ila mara kwa mara watatembelea kazi zao na ni mara kadhaa utawafuma wakiwa wanasoma kazi zako.

Hii inanifundisha kuwa kuna wakati ni vyema kusikiliza changamoto za watu na ukazilinganisha na plani zako na kisha ukayachukua mazuri na baadhi ukaachana nayo na kuendela na jitihada zako kwani kamwe hakuna atakayejua unafanya nini mpaka aone matokeo.

3. Ukichukua kazi ya mtu ukaiweka kwako inaweza kukubalika ila kwa kiwango kidogo kwani wengi walisha kutana nayo na ikakufanya kupoteza baadhi ya marafiki zako

lakini ukitulia na kutunga kitu kinachoendana na nini ulikiakisi kuandika hupokelewa kwa wingi na unaweza shangaa ikazunguka na kukurudia wewe mwenywe.

Hapa inanifundisha kuwa kila mtu anaweza kuuboresha mtazamo wake na kuongeza baadhi ya ubunifu na kuja na kitu kipya ambacho kitapendwa  na hapa nakubaliana kuwa kila mtu ana uwezo wa kufanya makubwa bila kuiga.

4. Kuwa blogger utapata marafiki kila siku wapya na wengi watakaa na wewe kufahamu unafanyaje kazi zako na kisha watapotea na siku unakuja kukuta kuwa nao ni mablogger na wenye kazi za ladha yako na wako juu.

Hapa najifunza pia katika maisha ni vyema kuwa mwangalifu wa mawazo yako na hata marafiki unaokuwa nao na kujitahidi kusoma nini wanataka kwako kuliko kuwa mwepesi wa kutangaza mipango yako.

5. Kuna baadhi ya watu wao watatumia kurasa zao na akaunti zao kukuzushia mambo mbalimbali ili tu ukwazike na hata kuamua kurudisha jitihada zako nyuma ili wasiwe na mpinzani.

Hapa najifunza kuwa ni vyema kuwa mvumilivu na usiwe mwepesi wa kutaka kubishana na kila kitu kwani muda unaotumia kufikiri, kuumia na kuliwazia hilo wenzako wanazidi kusonga mbele na ukija kushtuka muda umekwenda na wewe sasa umeshuka chini

Maisha ni zaidi ya somo la sayansi

You Might Also Like

0 comments: