Njemba lavamia Marathon likiwa na nguo za ajabu

05:44:00 Unknown 0 Comments


Mke mmoja alimwingiza njemba mmoja chumbani kwake wakati mme akiwa kazini, muda mchache baadae akasikia muungurumo wa gari kuashiria kuwa mmewe anapaki gari.

Kwa haraka akamwambia yule jamaa aruke dirishani, jamaa akasema umesahau nyumba yako in ghorofa mmoja au wataka nivunjike miguu? mke akawambia akija mme hapa atatuua wote jamaa kusikia hivyo akaruka haraka na kuanza kukimbia akiwa uchi na nguo mkononi.

Akiwa anakatiza mtaani akakutana na jamaa ambao wako kwenye mashindano ya mbio (marathon) ikambidi aungane nao kigumu huku wakimshangaa.

Mkimbiaji wa kwanza akamuuliza huwa mara zote unakimbia kwenye mashindano ukiwa uchi? Jamaa akasema ndio huwa napenda mwili uwe huru bila kubanwa na nguo

Mkimbiaji wa pili akauliza na huwa mara zote unakimbia na nguo mkononi? Jamaa akajibu ndio huwa napenda nikifika mwisho nivae na kurudi zangu nyumbani

Mkimbiaji wa tatu akamuuliza na je huwa unakimbia mara zote ukiwa umevaa condom? jamaa akasema ndio ila mara nyingi kama mvua inanyesha

You Might Also Like

0 comments: