Vita ngumu ya maneno kati ya mke na mme wa digital

15:43:00 Unknown 0 Comments


 Vita ngumu ya maneno kati ya mke na mme wa digital

Mke na mme walianza ugomvi na baadae kupelekea wao kuanza vita ya maneno kama ifuatavyo

Mke:

Niliandika jina lako mchangani nikafutika
Nikaamua kuliandika hewani likapulizwa na upepo,
Nikaliandika jina lako moyoni mwangu,
Nikapata ugonjwa wa moyo.

Mme:

Mungu aliniona nina njaa, Akatengeneza wali kuku,
Akaniona nina kiu, akatengeneza  Pepsi,
Akaniona nipo gizani, akaleta mwanga,
Akaniona sina matatizo, akakuleta WEWE.

Mke:

He he he, kweli akili finyu kama nyota ndogo za angani,
Unatakiwa ujijue na kujitambua wewe ni nani,
Na baada ya kujitambua utaelewa,
Hosptitali ya vichaa haiko mbali nawe.

Mme:

Mvua hufanya kila kitu kuonekana kizuri,
Hata majani na maua nayo hupendeza pia,
Na kama mvua huvifanya vitu vipendeze kwanini mvu a hii haikunyeshei wewe?,


Mke:

Mauaridi huwa mekundu, wakati maua mengine huwa rangi ya blue,
Nyani kama wewe unatakiwa utunzwe mbugani,
Usiwe na hasira kwani unaniona nami huko,
Sio kwenye zoo ila nikiwa nakucheka wewe

Nani kashinda??

You Might Also Like

0 comments: