Binti awachanganya abiria kwenye basi,,, abiria washindwa kuvumilia
Basi lilikuwa linatokea Mbeya kwenda Dar.
Ghafla binti moja aitwaye Antonia simu yake ikaita naye akipokea,"mpenzi niko njiani naelekea mwanza kwenye mazishi naomba unirushie salio tafadhali."
Baada ya kukata hiyo simu, simu nyingine ikaita naye akapokea tena,"My number one niko njiani naelekea Iringa kwenye graduation ya masters yangu, nitakupigia nikiwa pale, usisahau kunirushia ile hela kupitia simu nitaitolea huko nikifika lavu yuuu"
Baada ya muda kidogo simu nyingine ikaita tena naye akajibu,"Baba, niko njiani naenda Njombe kwa aliji ya enterview ya kazi nitakupigia baadae, hapa kwenye gari kuna kelele."
kijana mmoja aitwaye Macho ambaye alikuwa kakaa pembeni akamwita konda kwa sauti na kusema,"Kondaaaa!!! Kondaaaaa! Mwambie dereva asimamishe gari nishuke, kwani nyie na basi hili wapi mnaelekea!??"
0 comments: