Hausi boi kafanya yake ........ ndoa inatetemeka

11:47:00 Unknown 0 Comments

Jamaa karudi home usiku kutoka job akaenda chumbani kwa mtoto wake wa miaka sita kumtakia usiku mwema ila akamkuta mtoto wake kalala anatetemeka kama anaota ndoto hivi.

Ikambidi amuamshe na kumuuliza kama yuko sawa. Dogo akamwambia kwamba alikuwa anaota ndoto kwamba shangazi yake (yaani mdogo wake na mama yake dogo) amefariki. Dingi akamjibu: mwanangu lala, aunt yako mzima wa afya wala hana tatizo.
Dogo akalala. 

Siku iliyofuata kweli yule shangazi dogo aliyekuwa anamuota akadedi! Baada ya kama wiki hivi jamaa akaenda tena chumbani kwa dogo kumtakia usiku mwema akamkuta tena anaota ndoto nyingine na kuweweseka. Akamuamsha na kumuuliza tatizo ni nini. Dogo akajibu ameota kwamba babu yake mzaa mama amefariki. Dingi akamjibu kwamba babu ni mzima, yuko fiti na hana tatizo lolote. Dingi akasepa, dogo akarudi kulala. 

Kesho yake kweli babu akafariki!! Baada ya kama mwezi hivi jamaa kama kawaida akaenda tena chumbani kwa dogo kumtakia usiku mwema akamkuta dogo anaota na kuweweseka kama kawaida yake. Akamuuliza: tatizo ni nini mwanangu? Dogo akajibu: baba nimeota umefariki! Dingi kwa kujikaza akamjibu: lala mwanangu, hizo ni ndoto tu, mimi ni mzima wa afya, wala usiwe na wasiwasi. 

Kulipokucha dingi akaenda kazini kwa wasiwasi sana. Barabarani akaamua kwenda bila gari akihofia ajali! Siku nzima akawa hali anaogopa atawekewa sumu! Akawa akasikia kishindo anajificha chini ya meza ofisini kwa hofu. Jioni muda wa kutoka job ukafika dingi akarudi zake home. 

Kufika akakutana na mkewe, jamaa akaanza maongezi: mke wangu, leo siku yangu imekuwa mbaya sana! Mbaya mno! Na bado ni mbaya. Mkewe akajibu: Mimi yangu ndo imekuwa mbaya zaidi mpenzi. Asubuhi ile umetoka tu yule kijana wetu anayehudumia ng'ombe kaanguka hapo jikoni na kufariki hapo hapo!

share na like Tabasamu na Fuledi

You Might Also Like

0 comments: