Mchepuko wamchepua mlizi katika lindo..............................Aibiwa kila kitu

11:49:00 Unknown 0 Comments

Nilibahatika kupata kazi ya ulinzi katika kampuni moja maarufu kwa kuuza matairi ya magari mkoani Njombe.

Siku moja majira ya saa sita nikiwa lindoni na manyunyu yakipiga na ule ubaridi wa njombe ikanibidi niwashe moto ili niweze kuupasha mwili joto na usiku usiwe mgumu.

Nikiwa tayari nimewasha moto na ninaendelea kupata kajoto mara akaja binti mmoja mrembo haswaa, tena kavaa kisista du na akawa analalamika baridi na kuomba apate joto kidogo kwani kuna bodaboda ameiita ije imchukue...nikaona haina taabu nikampa ruhusa.

Dakika moja baadae akatoa sigara na kuniomba nimwashie, nikakataa na kumwambia awashe tu akasisitiza kuwa lile ni eneo la lindo na si vyema awashe yeye.
Nikaona ni sahihi kafikiria vyema nikaichukua na kuinama kwenye moto nimwashie.

Ile na inama nilipigwa bonge la ngumi ya utosi na kufunikwa na kitu usoni na ghafla sikasikia sauti za watu zikisema leta gunia na kisha wakaniweka kwenye gunia na  kunitupia kwenye gari ambalo nilisikia muungurumo likisogea.

Wakaanza kubomoa mlango na kulisogeza gari kisha kuanza kupakia matairi yote na kisha kuwasha gari na kuondoka na mimi nikiwa humo na kuwasikia kila walichoongea.

Gari likaanza kwenda mbio jamaa wakijisemesha, aisee dereva unakimbiza sana gari mara hii tunakaribia makambako?

Likaendelea kuzunguka huku wakimsifia dereva kuwa kalikimbiza sana gari yaani wameingia jijini mbeya mapema kuliko kawaida. Wakajadiliana na kisha wakafikia muafaka wanitupe sehemu iitwayo UYOLE, wakanitupa na kuondoka zao.

Asubuhi watu wakaanza kupita pale wanaulizana hili gunia lina nini sasa kwa kuwa mimi nafahamu sana kihehe nikaona niseme kwa kilugha, "Nene ndili munu" yaani mimi ni mtu.

Wakaniuliza, umetokea wapi? Nikawaambia mimi ni mwenyeji wa njombe, wakaonyesha kushangaa na kuniiliza tena, kwa wewe hapa uko wapi? Nikasema ni mbeya sehemu iitwayo uyole. Wakacheka bila kusema neno na kuondoka.

Dakika chache baadae nikabebwa na kupelekwa polisi na kisha kutolewa kwenye gunia.

Nikashangaa kumwona boss wangu bwana mwagito yupo nae pale kituoni akitoa maelezo ya kuibiwa na mlinzi kutoweka. Nikamuuliza boss umekuja saa ngapi hapa MBEYA?

Akanijibu kuwa haupo mbeya hapa ni njombe kituoni, baada kumsimulia wakacheka wote.

Kumbe wale wezi hawakusafiri kwenda mbeya wala nini, yaani walikuwa wakinizungusha mitaa ya njombe na kujifanya wanasafiri na kisha kunitupa pale pale njombe ili kunipoteza maboya.

Tangu siku hiyo nimecha ulinzi na hata nikimwona mtu anawasha sigara nakimbia nikijua nataka kutekwa na kuibiwa tena.

You Might Also Like

0 comments: