Mwandishi wa habari azimia kisa unoko

17:31:00 Unknown 0 Comments

MWANDISHI: Wewe unawalisha ng'ombe chakula gani?,
MKULIMA: Ng'ombe yupi Mweupe au Mwekundu?
MWANDISHI: Ng'ombe mweupe
MKULIMA: Ninamlisha nyasi na viguta vya mahindi,
MWANDISHI: Na mwekundu??
MKULIMA: vilevile nyasi na viguta vya mahindi,
MWANDISHI: ahaa sawa,na sehemu ya kulala ni wapi?
MKULIMA: Ng'ombe yupi mweupe au mwekundu?
MWANDISHI: Mweupeee!!!
MKULIMA: Mweupe ninamlaza bomani kulee,
MWANDISHI: na mwekundu?
MKULIMA: vilevile ninamlaza na mwenziwe!!!!
MWANDISHI: Hii sehemu yote majumba mengi,Na wakienda kulisha unafanyaje?
MKULIMA: Yupi mweupe au mwekundu?
MWANDISHI: Woooteeee!!!! {kwa hasira}
MKULIMA: Mweupe nina mfunga kamba na kumzungusha malishoni na kumrudisha,
MWANDISHI: na mwekundu vilevile?
MKULIMA: Mwekundu?,mwekundu ninamfunga kamba na kuzunguka nae kama mwenziwe!!!
MWANDISHI: Kwanini kila mara nikikuuliza huduma za ng'ombe zako unaniuliza mweupe au mwekundu halafu inatokea kuwa kazi zao wote ni sawa?????,
MKULIMA: Kwasababu Ng'ombe mweupe ni wangu,
MWANDISHI: Na mwekundu?
MKULIMA: Ni wangu vilevile!!!!!!heheheheheheheh.
{Mwandishi presha juu}

You Might Also Like

0 comments: