Ungekuwa wewe ungefanyaje?
Jamaa mmoja alihamia Tunduru kikazi, jamaa huyu alikuwa bachela Kufika huko akaanza kazi yake vizuri tu na kwa kua alihitaji kuwa na matumizi sahihi ya kipato chake hivyo akaamua awe anajipikia.
Kila siku alipomaliza kupika akijiandaa kula kuna paka mmoja akawa akimpigia kelele sana mpaka jamaa anaamua kumpakulia chakula yule paka.
Paka yule akazidi kumsumbua jamaa kwa tabia ile ya kupiga kelele na kula chakula kingi hivyo jamaa akaja na style mpya.
Siku moja jamaa akapika chakula chake wali nyama ya ng'ombe, na baada ya kupika akaamua aende zake akatembee ili aje ale
baadae yule paka akiwa hayupo.
Baaada ya matembezi ile anarudi ale akashangaa kuona yule paka kajipakulia chakula na yuko pembeni kashiba na kalala zake.
Duh jamaa akampiga yule paka mpaka akamvunja mguu wa mbele na kumtupa nje.
Asubuhi anaamka anasikia baba mwenye nyumba mkono wa kulia umevunjika.
Ungekuwa wewe ungefanyaje?
0 comments: