Binti akosa kazi kisa picha zake za fesibuku....... kazimia na ni siku ya nne leo haongei

11:20:00 Unknown 0 Comments



Dada mmoja mwaka 2007 akiwa chuoni mwaka wa pili alikuwa na akaunti ya facebook.

Akaunti yake aliitumia katika kuweka picha zake zilizomuonyesha huyu binti akiwa nusu uchi akijirusha na watu tofauti sehemu tofauti. 

Hata maneno mengi katika status zake hayakuwa ya kibusara zaidi ya matusi na kejeli za kudhalilisha watu.

Akaunti yake pia ilipata umaarufu sana na kila kijana alipenda kufuatilia matukio ya dada yule katika ile akaunti yale kila ilipoitwa leo.

Umaarufu wake ulizidi kukua kwani kupitia picha zile alipata marafiki zaidi ya kiwango na kuwa na followers wengi sana na mitoko ya kila ilipoitwa leo.

Mwaka 2011 aliamua kuifunga ile akaunti na kuamua kuwa na akaunti ya kistaarabu kwani sasa alishahitimu chuo na kukaa zaidi ya miaka miwili na nusu akikosa kazi ingawa kila alikoenda alionekana kufahamika kutokana na picha zake na mwishowe kuishia kukosa hizo kazi na kujipatia bwana.

Akaumia sana na kuamua kurudi kijijini kwao na kubahatika kupata kazi ya kujitolea katika taasisi isiyo ya kiserikali pale kijijini.

Wakati huo akawa kaachana na mambo ya mitandao na picha na kuwa mtu mwenye kujiheshimu.

Akapendwa kwa utendaji kazi mzuri na mwaka huu mwezi wa kwanza akafanikiwa kupata kazi katika NGO moja moja ambayo inajihusisha na kuwaandaa vijana kwa taifa lijalo lenye maadili mema.

Na kazi yake kawa program meneja na kupewa mkataba wa kulipwa 1,500,000/- kwa mwezi, kukopeshwa usafiri, malipo ya nyumba, matibabu, kuwekewa malipo ya baadae na marupurupu mengine mengi yanayoendana na majukumu yake.

Mwezi wa nne mwaka hu alitakiwa kwenda nchi moja ya ulaya magharibi kwa ajili ya mafunzo zaidi kuongeza ujuzi wake lakini safari hiyo imekatishwa baada ya blog moja kutumia moja ya picha kati ya zile picha zake za zamani.

Picha hiyo ikasababisha wakuu wake Kufuatilia na kuona picha nyingi zaidi za aina hiyo alizopiga huko nyuma zikiwa zimetapakaa katika mitandao tofauti na akaunti za watu facebook.

Kwa kuwa taasisi hiyo ni ya kidini dada amesimamishwa kazi kulingana na taratibu za ofisi yao.

Inaumiza sana kwani dada alishapata mwelekeo wa maisha yake mazuri lakini mambo aliyowahi kufanya huko nyuma leo yameharibu mkate wake na ndoto zake pia.

Rafiki unayesoma ujumbe huu, kumbuka kuna vitu unavyovifanya leo hapa mtandaoni iwe kwa kukusudia au kutokusudia vina athari kubwa sana kesho.

Kuna siku utakuwa baba au mama na hutaweza kumkataza mwanao awe alivyo kwa kuwa ameona jinsi wewe ulivyokuwa.

Inasemekana kumbukumbu za mtandaoni zinadumu sana na kwa miaka mingi, sasa kuna siku waweza poteza bahati nzuri kwa mambo uliyoyafanya leo.

"Kumbuka unachokifanya leo kina weza kukuwinda maisha yako yote na kukupotezea usingizi" 


Whatsapp 0713317171

(Picha haihusiani na tukio hili ni mfano tu)

You Might Also Like

0 comments: