Jeneza la kioo lawatoa nduki waombolezaji

10:34:00 Unknown 0 Comments




Enzi za ukoloni wakati dini inaingia mzee mmoja alitoka nchi za nje na kuja kuanzisha kanisa lake hapa bongo.


Akafanikiwa kulijenga kanisa kubwa sana na baada ya kukamilika akaanza kuwaomba watu wakasali kila mtu akawa anakubali kuwa atahudhuria ibada ila kila ikifika jumapili hawaendi.

Mzee yule pamoja na mkewe kila jumapili alipiga sana kengele ili kuashiria kuwa watu wanatakiwa kwenda kuhudhuria ibada lakini aliishia kuwapata watu wachachei au asipate kabisa.

Mzee yule aliumia sana na hakupenda kile kitendo cha kukosa ushirikiano kutoka kwa wale wenyeji ambao alifikiri wangekuwa waumini wake hasa kwa kuwa ndio walio muuzia kiwanja na hata kumsaidia kulijenga kanisa lake na pia kumwahidi kuwa wangeshirikiana nae katika ibada.

Siku moja asubuhi yule mzee akamuuliza mkewe," ni kwanini watu hawaji kusali?" Mke akasema kanisa lako limekufa na watu imani yao imekufa pia. Mzee akauliza tena, " je mtu akifa si huzikwa?" Mke akajibu ndio.

Basi mzee yule siku ile alipiga kengele kwa fujo tofauti na kawaida kuanzia asubuhi mpaka jioni, watu wakakusanyika pale kwa wingin wakimshngaa kwa nini ameamua kupiga kengele kwa fujo kiasi kile.

Mzee akawaomba samahani kwa kupiga kengele kwa fujo na kusema amefanya vile kwa kuwa amepatwa na msiba wa kanisa lake hivyo anaomba kila mtu ahudhurie jumapili itakayo fuata kwa ajili ya mzishi.

Jumapili ile kila mwenyeji alienda kanisani hasa akitaka kushuhudia kanisa litazikwaje. Mzee akaanza mahubiri akieleza ni kwa nini kanisa lake limekufa, na kueleza moja ya sababu ni kuwa limekosa waumini na kusema imani ya waumini nayo imekufa kama kanisa lake kwa hiyo wategemee misiba mingi.

Baada ya mahubiri yale akawaambia sasa kila mtu apite kumwona marehemu akiwa kwenye jeneza. yeye kwenye jeneza aliweka kioo sasa kwa kuwa wale wenyeji walikuwa hawjawahi kuona kioo kila mtu alipomwona marehemu alishtuka na kutoka nje mbio.

Huko nje wakaulizana wewe mwenzangu umemwona nani kila mtu akaanza kulia na kuhuzunika kwani yeye ndio alijiona kwenye lile jeneza kwni kioo kilimwakisi yeye.

Mzee alipowaomba wachukue jeneza wakalizike hakuna aliyesimama wote wakagoma wakihofia watajizika wao.

Na hapo ikawa mwanzo wa kanisa lile kupata waumini wengi kwani wote walihisi wangekufa

You Might Also Like

0 comments: