Mungu hapendi tabia hizi
1. Wewe wajua kabisa haujaokoka moyoni mwako ila umeamua kwenda kanisani na kujifanya umeokoka kumbe lengo lako ni kupata mchumba ~ tafadhali badilika MUNGU hapendi kutaniwa
2. Wewe unajifanya umeokoka ila kwenye daladala mtu akikukanyanga kidogo kwabahati mbaya,matusi yake hata shetani anashtuka ~ tafadhali badilika MUNGU hapendi watu kama wewe
3. Wewe kila siku kanisani hukosi na unajitolea sana ila pale nyumbani unakaa na mtoto wa mke mwenza na huishi kumpa mateso ya kufa mtu ~ tafadhali badilika MUNGU hapendi kutaniwa
4. Wewe ni mwanaume na unajua umeamua kuanza kuiimbia kwanya yako ya kanisa na lengo lako ni kumteka mtoto wa mchungaji ili umalize yako na kusahau kuimba ~ tafadhali badilika MUNGU hapendi kutaniwa
5. Wewe ni tajiri na una hela zako nyingi, kanisani watoa fedha nyingi na watu wanakusifia lakini jirani yako hapo nyumbani hana hata uhakika wa mlo wa jioni ya leo nawe hustuki kumsaidia ~ tafadhali badilika MUNGU hapendi kutaniwa
6. Wewe unajua kabisa ....... ongezea na wewe
0 comments: