Utani utani wapelekea binti kupoteza maisha..........kisa cha kweli
Marrysam: Tuonane basi mida hii nimekumiss mpenziFuledi: Sawa, Ila baadae kama mida ya saa sitahivi. Mida hii nipo na marafiki napata bia.
Marrysam: Mpenzi umeanza kunywa tena? /:
Fuledi: Ndio ila usijali sana mpenzi , Nitakucheki mida naona simu inataka kukuta chaji.
*Fuledi akazima simu yake kuepuka usumbufu wa kuchati na mpenzi wake*
Kisha akaendelea kunywa na marafiki zake na kujisahau mpaka ikafika saa kumi za jioni.
Ilipotimia saa kumi na nusu akarudi nyumbani na kumwona kaka yake akiwa kakasirika na amechanganyikiwa kama kuna kitu kimetokea vile.
Kaka akamwambia Fuledi," Nimepigiwa simu na watu wa hospitalini kuwa mpenzi wako amepigwa risasi na watu wasiojulikana na wamemwibia vitu na kukimbia na kumwacha akiwa ameshakufa, ULIKUWA WAPI FULEDI, SI ULISEMA UTAKUWA NAYE LEO?"
Fuledi akaanza kulia huku akiwasha simu yake na meseji zikawa zinaingia mfululizo toka kwa mpenzi wake alizotuma muda mchache kabla hajafa kwa kupigwa risasi.
1:45: Nilikuwa nimekaa nakusubiri hapa nyumbani kwako nje nafikiri sasa simu yako itakuwa imezima.
Naondoka nilitaka kukuona, Mpenzi enjoy na marafiki mimi naondoka nitext ukirudi nyumbani mpenzi....I Love you
1:55: Mpenzi kuna watu wananifuata nyuma yangu wananiogopesha sijui watanidhuru!
2:00: Ujumbe wa sauti*
Mpenzi naogopa wanazidi kunifuata katika uchochoro wa kutokea nyumbani kwako kwenda nyumbani kwetu, nifanyeje?
* Mlio wa bastola ukasikia * Mara kukawa kimya
Watu wengi tunatabia za kuwadharau sana wapenzi wetu na kujenga tabia za kuwapa marafiki muda mwingi kuliko familia au wapenzi wetu tulio nao.
Kama Fuledi asingeamua kuzima simu ili kuepuka kutumiwa sms na kupigiwa simu, naamini Marrysam ambaye sasa ni marehemu labda asingekutwa na majanga hayo.
Hebu tujaribu kuvikubali vitu ambavyo tumepewa, kwani huwezi ona umuhimu wa kitu ulichonacho mpaka kipotee.
Comment "Mimi namjali" kisha share kama kweli unamjali mpenzi wako. . . . .
Weekend njema
0 comments: