Changudoa alitaka kunifia kifuani

16:55:00 Unknown 0 Comments

Tuliachana na jamaa zangu baada ya kunywa nao pombe sana na wao wakawa wanawahi kuelekea majumbani mwao huku nami nikianza safari yangu kuelekea hoteli niliyofikia.

Kiukweli jiji hili nyakati za usiku kuna baridi fulani hasa kwa mtu ambaye umezoea kukaa katika miji ya joto kama vile sisi tuishio Dar.

Nikiwa kwenye gari nikajisemesha kuwa kwa baridi hii lazima nimtafute binti mmoja anipe joto la sivyo hali ingekuwa sio shwari na pombe zilishaanza kunipa ujasiri zaidi.

Nikampigia jamaa yangu na kumwambia ni wapi ningeweza kupata toto moja la kinyaki niweze jisitiri?

Jamaa akaniambia kuwa niende hangover bar pale lazima nipate utaratibu mzima na kukamilisha adhma yangu.

Nilifila hangover bar na kuagiza bia yangu huku macho yakitazama huku na huko na hatimaye nikamwona binti mmoja kakaa meza fulani akiwa peke yake.

Nikahamia pale na kukaa naye ila macho yake yalionesha kuwa mekundu na kama yamevimba nikahofia isije akawa ana ugonjwa wa macho

Swali langu la kwanza kwa mrembo ikawa ni kwanini macho yake yalikuwa vile. Akanijibu kuwa kichwa kilikuwa kimsumbua ila sasa kimetulia.

Baada ya kuridhika kuwa sio ugonjwa wa macho hivyo nikaomba nimpe kinywaji akakubali na maongezi yakaendelea.

Nilichokigudua ni kwamba alikuwa mgeni wa pombe na mbaya zaidi dakika chache nikaona kama zinataka kumchukua vile.

Nikamwomba tuondoke akakubali ingawa kukubali kule nilihisi kulikuwa kwa shingo upande ila ndio sikuwa na jinsi zaidi ya kumng'ang'aniza.

Tulifika pale hotel na akaniomba aingie kuoga ili aje mzee nifurahie malipo yangu, akaenda bafuni ila nilishangaa kwani alikaa zaidi ya saa bila kutoka huku kukiwa hakuna dalili za kuonesha kama angerudi.

Nikaanza kujichekea kuwa wanawake wa mji huu wana mbwembwe sana sasa mtu anaoga muda wote huo au anajichubua?

Nikaendelea kusoma soma mambo kwenye simu na story za fuledi kabla ya usingizi kunichukua kwa zaidi ya dakika 45 na nilipofumbua macho sikumwona pale.

Hofu ikanijia inawezekana kwa kuwa imekuwa mara yake ya kwanza kunywa pombe ukijumlisha na kujimwagia maji ya baridi basi yawezekana amezimia au hata kufa.

Nikajikuta naukimbilia mlango wa bafuni na kwa bahati nzuri haukuwa umefungwa na nikamwona akiwa kainamia sinki la maji huku akilia kilio cha chini chini na akifuta damu zilizokuwa zilimtoka puani.

Binafsi nikashtuka na kujiuliza nini kinaendelea na kupata ujasiri wa kumchukua na kumkalisha kitandani na kuuliza kipi kinachomfanya alie na kwa nini damu zamtoka???

Hakunijibu na kunuomba alale jambo nililomkubalia kwa shingo upande maana akili yangu ilikuwa muda huo kwenye ile issue ya a new device has been detected na  kunifanya nichukue konyagi yangu na kuigigida ili niukaribishe usingizi.

Ilinichukua muda na baada ya kick ile ya kinyagi hatimaye nikalala ingawa haukuwa usingizi wa kufurahia kama kawaida yangu.

Niliamka na kumkuta kakaa kwenye kiti akiniangalia sikumuuliza nini kilichomfanya alie jana ila nikachukua suruali yangu nikafungua waleti na kutoa noti 3 za elfu kumi na kumpa.

Akazipokea na kuziweka na mbaya zaidi badala ya kusimama avae nguo zake na kuondoka kama nilivyotaka afanye, akasimama na akavua kanga yale na kusema, "haya basi fanya ulichokusudia jana ili uridhike hela yako isipotee bure na vinywaji vyako nilovyokunywa"

Kwanza nilimshangaa na pili nikahisi kuwa dada huyu hakuwa ni malaya bali ana tatizo lililomfanya afikie hatua hiyo.

Nikamwambia mbona sijaongea neno mama? Wewe usijali kuhusu mimi, ni asubihi sasa na ni vyema ukawahi kwako.

Akaanza kulia tena jambo lililonifanya nichukie ingawa sikutaka kuonyesha. Nikamuuliza sasa tatizo ni nini, hela yako nimekupa tena zaidi ya uliyoitaka sasa walia nini? Niambie tatizo ni nini?

Akaniambia, " kaka nalia kwa nini nafikia kujiuza, kamwe sikuwahi kutegemea kuwa nitakimbia chuo ili nijiuze kumwokoa mama yangu ambaye anasubiri kifo kama asipookolewa na ndugu zetu wote wako mjini na hakuna hata anayeonesha dalili za kuokoa uhai wa mama aliyewapigania"

Kwani anatatizo gani na yuko wapi? Niliuliza

Akaniambia, "mama anasumbuliwa na saratani ya matiti na titi moja limrathiriwa na kama asipopelekwa hospitali kubwa na kukatwa basi kuna uwezekana mdogo sana wa kuishi zaidi ya mwezi?

Niliumia ingawa nikajifanya kukomaza macho lakini sekunde chache baadae nikajivuta kwenda bafuni.

Nikaufunga mlango na wakati huu machozi yalishuka kwa wingi na nikamkumbuka marehemu mke  wangu aliyefia ndani kwa kukosa msaada wa kupekekwa hospitali kisa wifi zake hawakumpenda na kumjulia hali mpaka anafia ndani.

Nikamfikiria binti huyu aliyeamua kujiuza ili tu mama yake asife nikaona ni upendo wa aina gani na kujitoa kwa namna gani huku.

Nikaufungua mlango na kuvaa nikamchukua na kuendesha gari mpaka kijijini na kumshuhudia mama yule akiwa katika maumivu na mateso makubwa sana.

Nilimchukua na kumpeleka mjini katika hospitali moja kubwa na alifanyiwa upasuahi haraka.

Niliendelea na kazi zangu huku nilimjulia hali yule mama mpaka alipopata unafuu kabisa ambapo wakati huo na mimi nilikiwa nimeshamaliza kazi yangu iliyonilpeleka katika mkoa huo.

Na hivi leo ni mwaka wa nne tangu nianze kumwita mama yule mama mkwe wangu.

Na kila nikikumbuka yaliyomsibu mke wangu huishia kutokwa na machozi kwani ni mke mwenye tabia njema, jasiri na asiye na makuu........na naamini kuna mabinti wengi ambao hujingiza katika biashara hii kwa kuwa wana matatizo na majukumu ambayo wanahitaji kuyatatua.

Mungu awape ujasiri wa kuamini wanaweza kuyakabili matatizo yao bila ya kutumia njia hii.

Share, commenr na like



You Might Also Like

0 comments: