MAMBO 19 AMBAYO KILA MSICHANA MWENYE UMRI KUANZIA 20 -29 ANATAKIWA AYAJUE (MUST READ)
1. Mpende na jivunie mama yako.
Jifunze kupitia makosa aliyo yafanya mama yako. It
hiyo itasaidia uishi vizuri kuanzia miaka ya 30.
2. Una uwezo wa kufanya vitu vikubwa kuliko unavyodhani. Huitaji kulala na Boss wako ili upandishwe cheo au kupata alama nzuri chuoni.
Soma usiku; jiwekee
extra time kwa ajili ya kusoma na kujua uwezo Wako ili uweze kufaulu
bila shida.
Hard work pays.
3. Wanawake sio viumbe dhaifu (weka akilini).
4. Unapokutana na Mwanaume kwa Mara ya kwanza akaonyesha kwamba anataka kukuvutia kwa fedha alizo nazo,
Hiyo ni hatari. Inawezekana ameshaoa anataka kulala Tu na wewe au bado ni mtoto achana nae.
5. Tengeneza ela zako mwenyewe. Anzia chini. hakikisha unapata fedha ambazo zinatosha mahitaji yako. Hiyo itakuondoa kwenye matatizo.
6. Unapokutana mwanaume wa maisha yako, usisahau kuvaa lile gauni lako la kawaida(lisilo la gharama) na ule mkufu Wako uliopauka na kupitwa na wakati(ukiona hiyo haimsumbui na bado yupo na wewe, basi anakufaa). ILA ukiwa unamsubiri mwanaume wa maisha yako atokee usilazimishe kujaribu kila mwanaume kuwa makini hapa.
7. Ujue mwili wako. Jiangalie mwili Wako juu mpaka chini kwenye kioo angalau Mara moja kwa wiki, ukiwa uchi na ukiwa umevaa nguo.
na ujue jinsi ya kuutumia mwili wako.
8. Maisha ni zawadi. Ila ili uweze kuifungua zawadi yako ni lazima ujue kipaji chako na uwezo Wako, usichelewa, Anza mapema.
9. Utoto umeisha ukiwa na miaka. Inapofika
20 inamaanisha uache utoto wote.Ila hii haimaanishi usifurahi, utaendelea kufurahia maisha yako lakini bila kushika uchafu.
10. Jitambue- kuanzia kuhakikisha nguo zako za ndani ni safi , kupika na
kujua kuishi na watu vizuri.
11. USITUMIE MADAWA (ya kulevya). Yanaua.
soma vitabu, utakua kifikra. Cheza kila upatapo muda kwa kadri iwezekanavyo utakua huru kiroho,
ndani ya moyo na mwili pia.
12. Urafiki unajenga daraja.
usisahau hii.
13. Kula kwa kuzingatia afya. Jifundishe kupika mwenyewe. Ukijua kupika itakusaidia sana mbeleni.
14. Usikate tamaa unaposhindwa.
jaribu tena. Usikate tamaa kwenye elimu/ kujifunza.
15. Acha Uoga. Uoga ni kitu unachoweza kukishinda kabisa, (kuwa na uoga ni ujinga)
16. Achana na vitu vilivyopita. huwezi kwenda mbele kama unaangalia nyuma.
17. Jifunze kusamehe, kuwa na upendo wa dhati na kuwa na roho nzuri na mcheshi kwa kila mtu, tena zaidi kwa watu wachini wale maskini wa kutupa.
18. We ni mrembo sana jinsi ulivyo. Usijilinganishe na watu wengine.
19. Usisahau kumuomba Mungu kwa kila jambo. Dream big today. usiogope kuzeeka, kumbuka kutabasamu kila wakati. Ishi maisha yako kwa furaha.
0 comments: