MUNGU ANAONA (KISA KIGUMU KUSOMA)

13:42:00 Unknown 0 Comments

Nilitembea hatua kama tatu toka nilipotoka pale kwa sonara na kujivuta mpaka chini ya mti mmoja wenye kivuli cha wastani na kuanza kujiuliza masawali mengi bila kuwa na majibu ya msingi.

Hivi ni mimi salome ambaye pamoja na utajiri wa mimi na mme wangu yaani leo nifikie kuuza mikufu na baadhi ya zawadi nilizonunuliwa na mme wangu eti nipate fedha ya kwenda kumnunulia dawa mme wangu? 

Kwa nini shemeji ameamua kuwa na roho mbaya kiasi pamoja na ukarimu wangu tena nguvu kubwa niliyoitumia kumshawishi kaka yake amlete kutoka kijijini na kuja kuwa meneja msaidizi wa kampuni ambayo mimi na mme wangu tumetumia miaka mingi, nguvu na fedha kuikuza na leo aniambie hakuna hata senti ya kuweza kumuuguza kaka yake na matusi juu yake?

Nikajisemesha kama tatizo ni mimi kutokuzaa basi wanihukumu mimi na sio kumwacha kaka yake ateseke katika kipindi hiki ambapo hana msaada wowote zaidi ya mimi nisiye na kitu na baba mkwe wangu ambaye hana uwezo wa kifedha na homa za uzee zikimnyemelea.

Nikapanda gari kutoka pale kijijini ambako shemeji aliamua kutumia nguvu kunipeleka mimi na mme wangu kijijini baada ya kudai hawezi kupona na tunatumia fedha za bure hivyo tukawa mzigo mpya kwa baba ambaye hakuisha kulia akiumia juu ya matendo ya kijana wake.

Nilifika mjini na kwenda ofisini ambako sikuonana na mtu zaidi ya kuchungulia kupitia dirisha na kuona meza ikiwa imetapakaa chumba za whisky kana kwamba ofisi imebadilika na kuwa chumba cha sherehe na wakati huo wa kazi hakuna mtu wa kuwahudumia wateja.

Nikarudi mpaka nyumbani ambako kwa mshangao ulioambatana na kilio cha chinichini nilishangaa kumwona shemeji yangu Dan akiwa katika kitanda cha mimi na mme wangu kalala na wanawake wawili wakiwa na chupa za bia na bila aibu akanitukana na kuniambia, 

"Wewe mwanamke tasa unafanya nini hapa badala ya kwenda kukaa na mmeo ambaye muda wowote atakuwa marehemu ?"

Yalikuwa ni maneno ya kawaida kwa upande wangu hasa kwa suala la kutozaa lakini kwa upande wa kaka yake nilishangaa dan kuongea manano yale kwa mtu waliyezaliwa naye tumbo moja na kuwa ni watoto wawili wa pekee wa baba mkwe wangu aliowakuza yeye mwenyewe baada ya mkewe kufariki wakiwa wadogo ambapo aliumwa na nyoka alipokuwa akitoka shambani kuwachimbia mihogo ya chai.

Sikuongea neno zaidi ya kwenda nyumba ya jirani kwa rafiki yangu ambaye pamoja na kunishangaa nilivyokuwa nimechoka na kuisha huku nikiwa nimevaa mavazi ambayo kiukweli hata wewe unayesoma usingeamini kama ni salome yule aliyesifika kwa urembo na kuwajali watu nilikopa shilingi elfu kumi na kuitumia kama nauli ya kurudi kijijini.

nilimkuta baba akiwa kamshika mme wangu akijaribu kumpa dawa kwani kichaa kilikuwa kimeanza kumpanda na kurupushani ilishakuwa kubwa nikamsaidia kumpa dawa ya usingizi na kisha dawa zake na ndipo nikamsimulia baba hali halisi ya mjini na jinsi dani alivyo.,

Maskini ya Mungu laiti ningelijua kuwa maneno yale yangeamsha matatizo makubwa yenye majonzi na simanzi hasa baada ya baba kukata roho masaa manne baadae tukiwa njiani kumpeleka hospitali baada ya bp kumpanda kamwe nisingeweza kumsimulia.

Lilikuwa pigo kubwa kwangu kwani sasa baadhi ya wana familia waliohongwa fedha na dan waliniweka kikao na kutoa maamuzi ya mimi kurudi nyumbani kwetu na kuwaachia kaka yao amabye mpaka muda huo hospitali zote zilikuwa zimeshindwa na kutuambia sasa liwe suala la kujikabidhi kwa Mungu.

Nilituma taarifa kwa baba yangu akaja kutoka kijijini na kunichukua baada ya kikao kizito cha tuhuma za mimi kuwa natumia madawa na pia sizai kwa kuwa madawa nimemfanyia mno mtoto wau ambaye ni mme wangu na tangu tumeoana nimekuwa nikileta mikosi katika familia yao pamoja na kusababisha kifo cha baba mke wangu.

Wakati huu machozi yalikauka na nilikuwa nikizimia mara kwa mara tangu pale kikaoni, wakati narushiwa nguo zangu na hata tulipokuwa niiani kurudi nyumbani kijijini bado hali yangu ilikuwa ni ya kuogofya ingawa namshukuru baba alinipa nguvu muda wote huo.

Niliporudi kijijini nilikuwa ni mtu wa kusali asubuhi mchana na jioni na nakumbuka nilisali mara nyingi kuliko hata muda nilioutumia kufanya mambo mengine pale nyumba na zaidi nikimwomba mungu amsaidie mme wangu apone na kurudi katika hali yake.

Siku moja nikakimbia na kwenda nyumbani ambako mme wangu aliwekwa na kwa kuwa walifunga mlango na hakukuwa na mtu niliruka kupitia ukuta na kuingia ndani ambako nilishangaa kuona mme wangu akiwa katika mavazi yta ajabu zaidi ya kichaa wa kawaida , hana dalili ya kuwa aliwahi kuoga na kama haitoshi chakula anawekewa kama mbwa pale nje.

Nilishindwa kujizuia nililia sana na kujibanza sehemu ambako nilimwona mzee mmoja mbaye alikuwa akija na kuvifuta vile vyombo kwa kitambaa kichafu na kisha kumweke chakula kichafu mme wangu na kuanzia siku hiyo nilikuwa nikijificha na kumpelekea chakula na kumlisha huku nikisali.

Ilipita miezi miwili nikiwa naendelea kufanya hivyo na kusali sana kanisani nikiwa peke yangu na namkumbuka siku moja nikiwa nasali kuna mama mmoja alinijia na kunipa chupa ndogo ikiwa na mafuta na kusema yatumie haya kupaka katika sehemu yoyote ya mgonjwa unayemwombea kwa siku tatu mfululizo.

WAkati ananisemesha mimi nilikuwa katikati ya sala hivyo sikukatisha sala yangu na nilipomaliza nilitoka nye kumwangalia mabacho kilikuwa kitendo cha dakika chache sikumwona na hata nilipouliza baadhi ya watu wakadai hawakumwona mtu pale.

Nilirudi nyumbani na kuanza kumpaka mme wangu mafuta yale huku nikisali kwa muda wa siku tatu na siku ya tatu jioni alikohoa sana na kisha akaanza kuongea na kuwa mzima kabisa.
Sitaki kueleza furaha niliyokuwa nayo japo mme wangu hakuwa naelewa kulichokuwa kikiendelea zaidi ya kuuliza alikuwa wapi. Siku tatu baadae nilishangaa shemeji dan akija na kulia akiomba msamamaha kumbe ndiyeb alikuwa nyuma ya vyote hivi kuanzia mimi kutokuzaa akidai hakutaka niwe na furaha na mpaka kaka yake kuwa kichaa ili amiliki mali yeye.


Siku tatu baadae dan alikutwa kajinyonga na mimi na mme wangu mpaka sasa tunaishi maisha ya furaha na amani huku tukizidi kumwomba Mungu atubariki  zaidi.

Mme wanfu alifanikiwa kuzirudisha biashara zake na anaendelea vyema wakati na mimi ndio namalizia kuandika habari hii feki nimtumie fuledi  ili jumapili iwe nzuri kwetu wote tutakao soma ..... 



You Might Also Like

0 comments: