Simu hii ya AJABU ikanza kuipoteza furaha ya baba pachu na hatimaye furaha ya familia nzima, kazini mpaka jamii inayomzunguka kuanza kumwona kama mtu anayeanza kuchanganyikiwa.

10:24:00 Unknown 0 Comments

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "



Yaliyomo

Baba Pachu ni kijana aliyejaliwa kuwa na mke na watoto wawili na familia yake imekuwa ya furaha na amani kwa muda mrefu.

Pamoja na kuwa na furaha hiyo pia Baba Pachu amejaliwa kuwa na mafanikio makubwa katika kazi zake binafsi na pia ni mfanyakazi wa kampuni moja maarufu sana yautafiti wa madini.

Siku moja akiwa katika mihangaiko yake binafsi nje ya jiji la Mbeya majira ya usiku akiwa chumbani mwake mara anapokea simu ngeni kutoka kwa mtu asiyemfahamu.

Mara ya kwanza ilionekana kama ni WRONG NUMBER lakini baada ya muda ulivyozidi kwenda ikaonekana kuwa sio WRONG NUMBER tena bali ni mtu anayemfahamu fika ingawa yeye hamtambui na nia yake ikiwa haieleweki.

Simu hii ya AJABU ikanza kuipoteza furaha ya baba pachu na hatimaye furaha ya familia nzima, kazini mpaka jamii inayomzunguka kuanza kumwona kama mtu anayeanza kuchanganyikiwa.

Baba Pachu anaanza mkakati wa kutatua tatizo lake na mkakati huo unamfanya baba Pachu kujikuta anapita katika njia zenye visa vya kutisha, majaribu, vioja na heka heka nyingine nyingi zenye maumivu na kuifunza jamii.

Futilia kisa hiki kila siku ya jumatatu mpaka ijumaa jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu na pia un aweza kupata kupitia whatsapp katika simu yako.

Kisa hiki kinakujia kwa udhamini wa A piece of cake party na  Gracious HOUSE of CAKES watengenezaji maarufu na waliobobea wa keki za aina mbalimbali kwa hafla mbalimbali waliopo jijini Mbeya na wanapatikana kwa namba 0767218014

Nawe waweza kuwa mdhamini wa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

You Might Also Like

0 comments: