Vifungu vya Biblia vilivyookoa jahazi
Jamaa: Hello mrembo, samahani, una mpenzi?Binti: Hapana. Sina mpenzi.
Jamaa: Kitabu cha Mwanzo 2: 18 "Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye."
Binti: Lakini mimi sikupendi jamani.
Jamaa: Waraka wa kwanza wa Yohana 4:8 "Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo."
Binti: Mh! Mi ntajuaje kwamba na wewe unamaanisha hayo maneno?
Jamaa: Injili ya Mathayo 12:34b "Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake."
Binti: Jamani leo kazi. Mi ntajuaje kwamba we ni mkweli na mwaminifu?
Jamaa: Injili ya Marko 13:31 "Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe."
Binti: Wewe! Na kwanini umekuja kwangu? Wasichana mbona wako wengi tu!
Jamaa: Mithali 31:29 "Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote."
Binti: We una mambo wewe! Sasa mimi kwangu umependa kitu gani?
Jamaa: Wimbo Ulio Bora 4:7 "Mpenzi wangu, u mzuri pia pia, Wala ndani yako hamna ila."
Binti: Mh! Huo uongo, mbona mimi hata sio mzuri kihivyo. Unaongeza chumvi tu!
Jamaa: Mithali 31:30 "Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa."
Binti: Nikisema nimekukubalia itakuaje?
Jamaa: Mwanzo 2:24 " Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja."
Binti: Jamani we mkaka. Inakuaje unajua maandiko kiasi hicho?
Jamaa: Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana."
Binti: Wowwww! Naona unampenda sana Mungu.
Jamaa: Zaburi 34:8 "Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini."
Binti: Mh! Haya bwana. Basi nipe muda nifikirie ombi lako.
Jamaa: Wafilipi 4:8 "Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo."
Binti: Mh! Jamani wewe, haya, nimekubali. Mpaka hapo nakupenda tayari!!
Jamaa: Ufunuo wa Yohana 22:21b "Amina"
0 comments: