Balaaaaaaaaaa
Saila aliingia dukani na kumkuta bwana chande akiwa kachanganyikiwa na wateja wengi hivyo nae akawa kwenye foleni ya kuhudumiwa.
Muda wake ulipofika akatoa noti yake ya shilingi elfu kumi na kuomba mahitaji yake ya nyumbani pamoja na vocha ya shilingi efu moja.
Bwana chande akampa mahitaji yake na badala ya kumpa vocha mbili za mia tano mia tano akajisahau na kumpa vocha mbili za shilini elfu tano na badala ya kumrudishia chenji ya shilingi 5000 akamrudishia tena shillingi elfu 10000.
Saila aliondoka akiwa anagundua kaongezewa tofauti na mahitji yake lakini akafurahi akijua kuwa kapata bila hata ya kuwa na roho ya utu na kuona ni kama dhuluma.
Siku nne baadae saila ambaye ni mfugaji wa kuku wa mayai aliamka asubuhi na mapema na kwenda kwenye banda lake ili aweze kuwalisha kuku wake na alishangaa kuona banda likiwa tupu yaani kuku wote wameibiwa.
Akiwa hajui nini afanye jioni ya siku hiyo mtoto wake alikuwa ametoka kuchukua fedha walizokuwa wakidai katika hotel fulani ambayo huwa wanapeleka na kulipwa baada ya siku kumi na nne mara mzee mmoja akaomba msaada wa chenji na mtoto yule kwa huruma akampa na alipofika nyumbani hela zote zilikuwa zimetoweka katika mkoba alioweka hela zake.
Siku zote mali ya dhuluma huwa haidumu na ni mikosi kwa familia au katika kukua kwako. Unaweza ukaifurahia leo na mwishowe ina majanga mazito na yenye kuumiza kuliko ulichokipokea kwa njia ya mkato.
Dhuluma sio katika fedha au mali tuu lakini dhuluma nyingine hutokana na kuwa wepesi wa kuahidi na mwishowe ukawa mtu usiye mtiifu kwa ahadi zako katika maisha ya kawaida, katika mahusiano na maofisini
Nakusihi jioni hii rafiki usomaye ujumbe huu Mungu akupe moyo wa ujasiri wa kujituma na kukufanya uyafurahie mafaniko yako huku ukipewa roho ya kuikimbia dhuluma kwani ni hatari na ina mwisho mbaya unaoambatana na bahati mbaya.
Kwa yule anayeichukia dhuluma na comment AMEN na kuushare ujumbe huu wa jioni
0 comments: