Post mbaya
Kuna wakati mtu unatakiwa kusimama na kufanya maamuzi magumu kwa mambo ambayo hapo awali ulidhani ungeendelea kuyakumbatia.
Hakuna hali mbaya na kuumiza ambayo inatakiwa kuwa sehemu ya mwili wako kwa maisha yako yote.
Kama umeanguka katika mapigano yako ya kimaisha haimaanishi utabakia kuwa hivyo maishani mwako.
Kama upo katika mahusiano magumu haina maana utaendelea kuwa hivyo siku zako zote.
Kwa kila jambo chungu amini kuwa kuna siku utaamka na kuona nuru njema iko mikononi mwako na kusahau machungu huku ukiwa na maisha mema ya furaha.
Sisemi kwamba hali hiyo itakuja tuu kama miujiza lakini itatokana na mtu binafsi kuchukua maamuzi magumu na kuamua kuibadisha furaha kuwa furaha endelevu na huzuni kukoma na kugeuka kuwa furaha kwako.
Lazima tujifunze kuyakataa yale yaliyotuumiza na kuendelea kutufanya kukosa ujasiri wa kusimama na kuonesha furaha zetu.
0 comments: