Facebook ilivyonikosesha raha (Sehemu ya pili 2)
17:00:00
Unknown
0 Comments
17:00:00 Unknown 0 Comments
Facebook ilivyonikosesha raha (Sehemu ya pili 2)
Ilikoishia jana
Jumamosi ilivyofika nikaamka mapema na kuwahi ofisini ili nimalize majukumu yangu mapema na niweze kwenda kwa binti Coletha.
NIliwasili mapema kabla yake eneo la miadi na nilipofika pale mhudumu alinifuata na kuniambia kama mie ni mgeni wa Coletha na nikamkubalia kwa kutikisa kichwa na baada ya hapo akanichukua mpaka alipokuwepo Coletha.
Endelea
Ile naufungua mlango niweze kumwona yule binti, mara moyo wangu ulinipasuka na kujikuta nikitamka kwa haraka " hapana haiwezekani" na hata nilipoulizwa na mhudumu kulikoni sikuweza kuongea chochote zaidi ya kujitupa kwenye kiti pale chini.
Wakati huo jasho lilianza kunitoka na nikawa najiuliza ni kwa nini niliamua kuwasiliana na mtu huyu. Nikiwa katikati ya mawazo hayo alisimama binti huyo na kuja mpaka nilipokuwa nimekaa.
"Mbona umeshtuka sana Fred? au hukutegemea kuwa tutaonana?"
Swali hilo lilizidi kunichanganya kabisa kwani mtu huyu simfahamu na alikuwa tofauti kabisa na binti niliyekuwa nikichati nae tangu siku ya kwanza aliponi-poke au kama watoto wa mjini wasemavyo alivyonitekenya.
Kiukweli pamoja na kuwa nilishakuwa nimehudhuria gym kwa karibu miezi miwili na mafunzo ya karate yaliyonipa ujasiri wa kukabiliana na vibaka wa mwanjelwa lakini hofu iliyonitawala muda huo ilizidi ile ya kumwona simba.
Nasema hivyo kwani binti yule sikujua ni nini kilichokuwa kinampa hali ya kuogofya mpaka nikatoa ile sauti ya mshangao, na pili iweje awe ni tofauti na yule niliyechati naye kwa muda wote huo na kunifahamu vilivyo?
"samahani dada nafikiri nilikuwa nachati na mtu tofauti na wewe kwani yeye anaitwa coletha, je wewe unaitwa nani?" Ilinibidi nijitose kusema hivyo ili angalau nianze kuyazoea mazingira.
" Usijali Fred, kwanza naomba unisamehe na tafadhali usinyanyuke na kuondoka kama unavyokusudia kufanya, nitaomba unipe japo dakika niweze kujitambulisha vizuri" alisisitiza dada huyo huku akishushia na funda moja la juice iliyokuwa mezani na kuendelea kusema.
"Fred nimekuwa nikifuatilia sana post zako na nimekuwa nikiona jinsi watu wanavyochangia na kurfuahi nawe, hivyo nikajikuta natamani kukufahamu na niwe mkweli kuna akaunti niliwahi kuitumia kuchati nawe lakini kuna ujumbe mmoja nilikutumia ukakuudhi na ukaniblock lakini nikaonaa ni vyema nije nikae na wewe na kuomba samahani hivyo nikatumia akaunti nyingine na kutumia jina la coltha........."
"jina lako la mwanzo lilikuwa lipi?" nimlimdakia hata kabla ya kumaliza maelezo yake ili kujua ni jina gani alikuwa akilitumia kwani mimi nina zaidi ya watu 135 nimewablock ili nimejue vizuri na nijue kudeal nae
"Samahani tena Fred, sitapenda ufikie huko ila naomba ujue nimependa zaidi tuwe marafiki mpenzi wangu Fred" alimalizia kuongea maneno hayo huku akitaka kunikumbatia lakini nikajivuta haraka na kumwambia atulie mimi ni mme wa mtu na nina jiheshimu.
Kweli dada yule alisogea pembeni na wakati huo mhudumu akawa amekuja na hata alipotaka kunihudumia nikajikuta nikigoma na kwenda mwenyewe mpaka kaunta ya nje ili nijinunulie kinywaji mwenyewe kwa kuhofia wasije kuwa wameweka limbwata au kuna mchezo.
Nilirudi pale ndani na kunywa maji yangu niliyonunua kwani sikutaka kunywa bia nikihofia pia zisije nichukua nikanasa kwenye mtego wa mwovu shetani aka cothetha maana nilihisi kama ni mtego.
Tuliongea kwa muda ingawa kiukweli hakunifanya nifurahie mazungumzo kama nilivyoamini kuwa coletha angekuwa na sikutaka tena kujua jina lake halisi.
Lakini kuna kitu nikiwa pale nilianza kukihisi hasa kila nilipoyachungulia macho yake na kila muda ulivyozidi kwenda nikajikuta nikizidiwa kama vile mwili hauna guvu au kama nimelewa vile yaani sikujua chochote.
Nakuja kuamka nikajikuta nipo...........................................................
Nitaendelea kesho mida kama hiii, unaruhusiwa kutembeleawww.karibumbeya.com

Fuledi Mwagito
Nakushukuru kwa kunipa nafasi hii adimu sana ya kufurahi, kuelimika na kubadilishana mawazo. Nitafurahi sana kama utaniachia comment hapo chini ili nijue kama habari,ucheshi, simulizi na vioja vioja hivi vimekupa siku yako kuwa BOMBA. Kumbuka nawe waweza share nami chochote ulichonacho kwa kunicheki kupitia whatsapp kwa namba 0713317171 au kupitia comment. Asante.
0 comments: