Kama wewe ni SINGLE MOTHER popote pale ulipo

22:32:00 Unknown 0 Comments

Kama wewe ni SINGLE MOTHER popote pale ulipo bila kujali
Mwanaume alikukimbia na mimba yako na sasa uko peke yako au una Mwanaume yupo ila ndio vileeee yupo kama jogoo la kuchora halidonoi wala haliwiki...CHUKUA SHIKAMOO YAKO!!
Kama wewe ni mjane na umebaki na jukumu lote la kulea mtoto/ watoto...nasema chukua shikamoo yako
Kama wewe mwanadada uliamua tu kuzaa na kulea mwenyewe pasi kujali kukimbizana ustawi wa jamii kushikana mashati juu ya pesa ya matumizi...naomba chukua saluti yako!
MALEZI YA MTOTO YA KULEA PEKE YAKO KAMA MWANAMKE... NI UJASIRI WA HALI YA JUU!!...usijali watu wanasema nini juu yako, usijali wenye wenzi wanakuhukumu vipi, usijali jamii inakuona mkosaji vipi... kazi unayoifanya hata Mungu anajua ni ngumuuuuuu!!... na wapo wengi tu waliofanikiwa maisha wametoka mikononi mwa single mothers!
Umesikia!!....



Karibu Mbeya shared a link.
Posted by Fred Kihwele · 4 hours ago
200 people reached

You Might Also Like

0 comments: