Kuna wanaume wana uchu sana na wanawake

16:39:00 Unknown 0 Comments

Sikuwahi fikiria kama kuna siku ningefanikiwa kumpata mtoto mwenye uzuri, umbo na rangi
kama ile kabisa maishani mwangu lakini yamenikuta.
Juzi nikiwa natoka zangu town mnyaki nature rafiki yangu wa ukweli akanipigia simu kuwa
yupo maeneo ya nyambono na kuniambia nikamcheki mara moja kwa ajili ya lunch.
Nikiwa njiani nikamng'aza bibie mmoja mwenye swaga za kudatisha na hatimaye akaniteka
taratibu.
Nikashuka kwenye daladala na kumfuata na kumpa mwaliko wa lunch akasita sita ila kutokana na kusisitiza kwangu hatimaye wote
tukaelekea nyambono.
Baada ya kufika nyambono Bar nikamkuta Suphian na kama kawaida yetu story zikaanza
pale huku bia zikishuka kwa fujo na binti taratibu akawa kaanza kuyakubali mapigo huku akiwa
anamtafuna ndege mmoja maarufu kwa jina la kuku.
Si wajua tena vijana wa sasa pale kila simu iliyoingia iliongelea fedha tu na lengo kumfanya mtoto azidi kudata.
Meza ya jirani karibu na mlango walikuja na kukaa majamaa fulani ambao sikutaka kuwafuatilia sana ila ukiona vifua vyao lazima ujue wananyanyua vyuma au matairi ya trekta.Baada ya kufurahi pale tukaamua tuhame kiwanja twende pande mpya.
Tukawasha gari la suphian na kwenda mitaa ya mbalizi. Na tukaendeleza bia mwendo mmoja.
Haikupita dakika chache gari moja ikapaki pale na wale majamaa tuliokaa nao meza ya jirani kule bar wakashuka pale.
Mmmmh mie machale yakaanza kunicheza nikamwambia jamaa tuondoke nimeona kama
twafatiliwa vile. Ingawa naona binti kama hashtuki vile.
Ile twataka kusimama tu jamaa wakaja na kusema hatoki mtu hapa.
Mimi nikaanza kutetemeka pale lakini jamaa wale wakasema msijali wakaagiza bia, mie nikaanza kuhofia nisije wekewa sumu pale lakini wale jamaa wakaniita nje na kusema kaka yaani wewe kula pombe usijali....tunafuraha sana
tulitaka tujue nani anatembea na dada yetu maana tangu aambukizwe UKIMWI watu
wamekuwa wakimkimbia na yeye anakosa raha kwani hana mtu hivyo wewe ni shujaa.
Jasho la uoga wa kifo likaanza kunitoka upya na safari hii ni hili la NGOMA, nikamwita suphiani na
kumwambia kuwa kumbe hawa ni kaka wa binti na wanadai binti kawaka........tukatafuta upenyo
na kuwakimbia.
Nusu saa baadae yule binti akatupigia mbona nyie sio wastaarabu? Yaani mmenileta mbalizi na kuniacha na hawa jamaa zenu kulikoni?
Baada ya kuongea nae na kumwelewesha kuwa walidai kuwa ni kaka zake binti akacheka na
kudai duniani akili wale mlipoondoka wakaanza kunipa sound wananitaka pia.......sio kaka zangu ila wamewazidi ujanja.
Nimeishiwa nguvu naona majanga hayaniishi...
Sasa mtoto nimemkosa na ananiona mie mwoga


You Might Also Like

0 comments: