Ukisikia tabia njema yalipa ndio hii hapa
Jana majira ya saa mbili na nusu asubuhi ilinibidi nitoke nyumbani na kwenda kwenye mishe mishe zangu kama kawaida yangu.
Kwa kuwa ni jumatatu nikaona wacha nianzie bank niingie ndani na kuona kunani kwenye akaunti yangu hasa ukizingatia nilikuwa nimepoteza kadi yangu.
Fuledi mara zote huwa mcheshi na humzoea mtu haraka sana basi kuna mama mmoja yeye
alikuwa mbele yangu na alikuwa akifurahia vituko na hadithi ambazo tulikuwa twataniana
mie na baadhi ya marafiki ambao tulikutana pale.
Baada ya kumaliza shida zangu natoka nje naona yule mama anaondoka na gari yake na pembeni kaacha fuko kubwa ikanibidi niukimbilie fasta kabla mtu mwingine hajaona.
Kufika pale kuufungua sikuamini kuona minoti ya kumi kumi na tano yakiwa yananichekea, kwa
akili ya haraka ikanibidi nitoke haraka na kudaka bodaboda na kumwambia dereva tulikimbize gari
aina ya benzi ambalo limetoka hapo punde likiwa laendeshwa na mama.
Boda boda yule alienda spidi sana na baada ya dakika chache tulimkuta yule mama akiwa
kwenye foleni na baada ya kumwonyesha ishara ya kisimama yule mama naye akapaki gari kando
na kisha akasimama.
Nikamwonyesha ule mfuko yule mama hakuamini kwani naye alijua uko ndani ya gari na kwa madai yake ile hela isingefika kwa mdeni wake ndani ya muda mchache ujao basi nyumba yake ilikuwa ipigwe mnada.
Hakuwa na mengi akamlipa yule bodaboda na kumwambia anirudishe kwangu na mimi nikamwachia namba ya mtaa ninaokaa pamoja na mawasiliano yangu.
Njiani wakati narudi yule boda boda akaendelea kunipa maneno mengi balaa mara umechezea bahati ooooh mara sijui wewe mshamba wa wapi sijui.
Sikumjibu chochote zaidi ya kukaa kimya mpaka aliponishusha nyumbani.
Masaa matatu baadae mdogo wangu wa mwisho akaja kuniita akisema kuna mgeni ananiulizia ile
kutoka nikakutana na yule mama aliyesahau fuko la hela akiwa na kabahasha akanikabidhi nikiwa bado nakashangaa na sijafungua
akaniambia ile bahasha ina cheki yenye milioni kumi na tano za kuanzisha biashara na pia
amenipa gari aina ya Alteeza kwa kuwa nimemfanya aamini vijana wa kitanzania wana tabia nzuri kupitia kitendo chagu.
Kiukweli nilipiga kelele za furaha mpaka majirani wakaja kushuhidia.
Furaha iliishia pale wife alivyonishtua hey Fuledi mbona unapiga kelele mie nakuamsha uje ule ugali tayari Duh sikuamini kama ni ndoto za mchana.
Nimeurudia umaskini wangu na hapa naendelea kula ugali wangu na maharage..... Maisha haya
ni kuwa na imani
Ha ha ha ha ndoto mbaya sana
7 people reached
0 comments: