Mme amfundisha mke jinsi ya kupika mayai

13:56:00 Unknown 0 Comments

Mke alikuwa anatengeneza mayai ya kukaanga kwa ajili ya chai ya asubuhi.
Mara mme akaingia jikoni na kuangalia mke akiwa anakaanga yale mayai.
"Tafadhali pika taratibu,"akasema mme, "Taratibu”! Ongeza mafuta yai litaungua! Mungu wangu yaani unapika mayai matatu kwa mkupuo??.
Ni mengi mno! Yagueze sasa, fanya
haraka yataungua!

Yageuze mayai plz! Haya ongeza tena mafuta.
Mungu wangu! Sasa mafuta ya kuongezea utayapata wapi?
Yataungua tu lazima.. Tafadhali! Nimekuambia yageuze taratibu!
Huwa hupendi kunisikiliza ukiwa unapika!!!!

kwanini??? Kamwe hiniskilizi!
Geuza tena!
Umechanganyikiwa??? Mbona sikuelewi wife nisikilize?
Usisahau kuangalia kama chumvi imekolea.
Unajua huwa unasahau mara nyingi. Tafadhali weka chumvi!!! weka chumvi!!! weka chumvi!!!
Mke akaacha kupiga na akamwangalia mme kwa
muda kisha akasema. "Una tatizo gani wewe?

Unafikiri mimi siwezi kupika mayai mengi kwa pamoja?"
Mme kwa upole akamjibu mke "Nilitaka uone jinsi gani wewe huwa unaongea nikiwa naendesha gari."

You Might Also Like

0 comments: