Mwandishi mwenye kiherehere azimia asubuhi hii kisa udadisi
MWANDISHI: Wewe unawalisha ng'ombe chakulagani?,
MKULIMA: Ng'ombe yupi Mweupe au Mwekundu?
MWANDISHI: Ng'ombe mweupe
MKULIMA: Ninamlisha nyasi na viguta vya
mahindi,
MWANDISHI: Na mwekundu??
MKULIMA: vilevile nyasi na viguta vya mahindi,
MWANDISHI: ahaa sawa,na sehemu ya kulala ni
wapi?
MKULIMA: Ng'ombe yupi mweupe au mwekundu?
MWANDISHI: Mweupeee!!!
MKULIMA: Mweupe ninamlaza bomani kulee,
MWANDISHI: na mwekundu?
MKULIMA: vilevile ninamlaza na mwenziwe!!!!
MWANDISHI: Hii sehemu yote majumba mengi,Na
wakienda kulisha unafanyaje?
MKULIMA: Yupi mweupe au mwekundu?
MWANDISHI: Woooteeee!!!! {kwa hasira}
MKULIMA: Mweupe nina mfunga kamba na
kumzungusha malishoni na kumrudisha,
MWANDISHI: na mwekundu vilevile?
MKULIMA: Mwekundu?,mwekundu ninamfunga
kamba na kuzunguka nae kama mwenziwe!!!
MWANDISHI: Kwanini kila mara nikikuuliza
huduma za ng'ombe zako unaniuliza mweupe au
mwekundu halafu inatokea kuwa kazi zao wote ni
sawa?????,
MKULIMA: Kwasababu Ng'ombe mweupe ni
wangu,
MWANDISHI: Na mwekundu?
MKULIMA: Ni wangu vilevile!!!!!!h
eheheheheheheh.
{Mwandishi presha juu}
Karibu Mbeya shared a link.
www.karibumbeya.com ni tovuti namba moja mkoani Mbeya inayokupa nafasi ya kutangaza biashara na huduma yako BURE na kuwafikia watu wengi zaidi ikiwa ni pamoja na kukupa nafasi ya kufahamu huduma na bidhaa zinazopatikana Mbeya kwa urahisi kupitia mtandao
Jisajibu bure kwa kuibofya link hii http://karibumbeya.com/register/
Jisajibu bure kwa kuibofya link hii http://karibumbeya.com/register/
10 people reached
0 comments: