Post ambayo marafiki wengi hujifanya hawaioni
Neno la LeoMarko 11:25-26, Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. [Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.
TAFAKARI: Kuna maombi mengi katika maisha ya watu hayajibiwi sio kwa sababu ya dhambi au shetani ana nguvu sana bali ni kwa sababu kuwa wengi hawajasemehe.
Kuna wengi wetu tunaishi na vinyongo vya watu ndani mwetu, tuna mengi tumeyabeba na kuna uchungu wa mambo mengi ambao hatutaki kuachilia.
Hii imepelekea maombi yetu kutojibiwa maana kutosamehe ni jambo mojawapo inayopelekea kutojibiwa maombi. Samahe leo hii.
SALA : Mungu wangu na Baba yangu, naomba unipe neema ya kusamehe na kuachilia katika maisha yangu. Nisadie nisamehe hata yale ambayo vidonda vyake bado vibichi mpaka leo ili na wewe upate kunisamehe. Kwa Jina la Yesu, Amina.
0 comments: