NJia mpya na bora ya kuulinda moyo wako uliumizwe

09:58:00 Unknown 0 Comments

Ulinde sana MOYO wako 

Kama utafanikiwa kuisoma hii na kuitumia naamini ina uwezo wa kuchangia katika kuyabadili maisha yako… 

Nimewahi sana kuamka siku ya leo na kujifungia sehemu nikiwa busy nasoma na kuzihariri baadhi ya kazi zangu. Naupenda ukimya wa alfajiri kwani Napata nafasi pia ya kufikiri mengi na kuongea mengi moyoni mwangu na hata kujisemesha kwa sauti ya chinichini kwa imani ya kuwa Mungu ananisikiliza. 

Nimetamani nikushirikishe na wewe uone somo ambalo nimelipata na kujifunza pia.

Ufunguo namba moja katika kukufanya uyafikie mafanikio yako ni kuhakikisha unaulinda tena unaulinda sana moyo wako. 

Sasa, mtu anavyokuambia uulinde moyo wako anakutaadharisha na kujiweka katika hali au kukubali hali zitakazokufanya uumizwe moyoni wako kutokana na watu au mambo yanayoweza kukufanya uwe katika hali ya msongo wa mawazo ikifuatiwa na simanzi na kasha kuumiza moyo wako pia. Pamoja na jambo hili ya moyo kuwa na upana wake katika kuliongelea lakini sitataka kuingia ndani sana .

Wakati tunazaliwa tuna kuja tukiwa na moyo ulio safi kabisa na usio na doa au jeraha la aina yoyote ingawa tunavyozidi kukua mioyo yetu hubadilika kutokana na mambo mbalimbali pamoja na watu tunaokutana nao kila siku yani changamoto za maisha kwa ujumla.

Najua fika kuwa hatuwezi kuitunza mioyo yetu ile ya udogo ikakua ikiwa hivyo maisha yetu yote, hasa baada ya kujikuta katika hali ngumu za kimaisha kama vile kudanganywa, kusalitiwa, kutumika vibaya, kudhalilishwa, kuumizwa na hata kufanyiwa mambo magumu. Niamini kuwa unaelewa ninachokimaanisha pia kwani hata mimi naandika hivi nikiwa na mifano hai hasa katika baadhi ya mambo niliyoyapitia katika maisha yangu na kujikuta nikiumiza moyo wangu kuanzia suala la mapenzi, ushirikiano, kazi, marafiki hata biashara.

Nimewahi kuyapitia hayo kwa maumivu ya aina yake ambayo kwamwe sitataka kuyasimulia kwani niliyasahau na kuamini sasa mimi ni Fuledi mpya, na kama nawe umeshawahi kuwa na uzoefu na maumivu hayo basi tupo sawa ila kama muda huu uko katika hali kama hiyo niliyowahi kukutana nayo ya kuumizwa moyoni basi kuna mambo mawili muhimu sana ningependa uyafahamu asubuhi hii.

Jambo la kwanza, jifunze somo lililopo ndani ya kuumizwa huko na kuona ni kwa namna gani utaweza kujitoa na kurudi kuwa mzima ukiwa na moyo wako ulio salama huku ukutumia muda mchache kuponyesha mjeraha yako. Kwani baada ya kuligundua hilo utaweza kusamehe kila lililokusababishia maumivu hayo na kusimama tena.

Jambo la pili, hutakiwi kumwacha mtu huyo, watu hao au hali hiyo kukufanya uubadili moyo wako na kuwa tofauti na ulivyokuwa hapo awali.

Naamisha nini ninavyosema hivyo?

Kama wewe una moyo wa kusaidia watu wengine yaani mtoaji na umeumizwa na watu ambao uliwasaidia na wakafanya visivyo basi usiache kutoa tena……………..ila saidia watu wengine wenye uhitaji zaidi.

Kama wewe ni mtu unayewapenda watu na kuna watu wanakuchukia na kukumiza basi wewe usiache kuwapenda…. Wapende watu wengine wanaopendeka. Kwani kuna siku utafanikiwa kukutana na watu wanaoutambua na kuuthamini moyo wako wa upendo au moyo wako wa kujituma.

Kumbuka hili, watu wengi wamejikuta wakifanywa kuwa na mioyo inayokataa kuwa na usafi au usalama ndani yake na hawawezi tena kujikubali kuwa na mioyo isiyo na jeraha na mara nyingi sio makosa au makusudi yao kuwa hivyo.

Hayo yote yanatokana na magumu waliyokutana nayo katika maisha yao na kuwafanya kuwa na mioyo hiyo. Kwa upande wako usijaribu kukubali wakubadili pia. Kuna watu wengi watakuumiza na kuukataa moyo wako wa ukarimu na upendo, na hata ikitokea wakakukataa basi wewe usibadilike au kuumia kwa muda mrefu. 

Hebu jifanye wewe ni Yule Yule na tafuta nafasi ya kuangalia upande wa pili na kuwa ana furaha zaidi kwani kuna watu wengi bado wanakusubiri na wanauthamini huo moyo wako.

Kwa nini ni muhimu kufanya hivyo?

Kwa sababu Mungu anakubariki wewe kwa jinsi moyo wako ulivyo. Kama wewe moyo wako ni wa ukarimu na upendo, utoaji na unagawana kile ulichonacho na wengine bila kuwa na jambo unalolitaka au kuliwinda kutoka kwao kama malipo ya utoai au upendo wako kwao, basi huo ndio moyo ambao Mungu anataka kuubariki muda muafaka ukifika.

Kama utaubadili moyo wako na kuwa tofauti kisa watu walikuumiza basi kumbuka umekipoteza kitu ambacho mungu alitaka kukibariki kutoka kwako, hivyo usikaribishe watu kuumiza moyo wako na ukabadilika kwani utapoteza Baraka nyingi kwa kufanya hivyo.

Nakutakia kulike kwema kwa Karibu Mbeya


55 people reached

You Might Also Like

0 comments: