Binti katili kuliko wote
Wengi wa marafiki zangu pamoja na wanafamilia wangu walisema niache ujinga kwa kuwa ni utoto au nawaza ndoto za mchana.Nilibishana nao na kuwambia kuwa mimi na Antonia ni zaidi ya wapenzi na kuwa tunatarajia baada ya miaka kadhaa kuja kuwa na familia moja kwa hiyo sioni cha kunifanya niache mpango wangu wa kumsomesha shule Antonia wangu.
Maneno hayo niliyaongea kwa uchungu na hisia kubwa za mapenzi yenye msimamo baada mimi kufeli mtihani wa kidato cha pili na Antonia kufaulu huku baba yake akifariki ghafla kwa kifo cha ajali ya bodaboda na kishindwa wa kumsomesha tena.
Nikawaambia mimi kichwani sina uwezo wa darasani ila kwa kuwa Antonia ambaye wengi waliyafahamu mahusiano yetu na yeye yupo safi kichwani na hana wa kumsomesha mimi nitafanya kazi zangu huku nikimlipia ada ya shule na kumwanda mke wangu mtarajiwa.
Niliamini nitaweza kwani muda huo shamba langu la vitunguu lilistawisha vyema na kuchukua baadhi ya mavuno na kulipa kila kitu kwa ajili ya mahitaji ya antonia
Kila mtu alishangaa na nakumbuka wakati Antonia akiwa mwaka wa mwisho pale shuleni kidogo azimie kwa furaha baada ya tafrija fupi ya sapraiz kwa ajili yake na ilifika kipindi mbele za watu alisema na hapa na mnukuu,
" Maisha hayatakamilika kamwe bila ya mpiganaji wangu na mme wangu mtarajiwa aliyenipenda nami nikampenda tangu siku ya kwanza twaonana na kucheza kama watoto mapaka leo tupo wote"
Matokeo yakatoka na Antonia akafaulu nami nikanpeleka shule moja ya wasichana mkoani mbeya na kwa bahati mbaya matokeo hayakuwa mazuri sana kwa hivyo hakupata ufadhili wa masomo chuo kikuu.
Kwa mapenzi ya dhati na kwa kuzingatia mimi sina elimu ya kutosha nikaona ni bora mama akiwa msomi katika familia hivyo nikaongea na jamaa yangu ambaye alifanikiwa kumtafutia chuo kikuu cha Dar aka UDSM.
Akaingia kama mwanafunzi wa kujilipia nami nikakazana na kilimo na kuhakikisha nampangia chumba pale shekilango karibu na bar maarufu ya dagaa dagaa na kuhakikisha napata elimu kwa kumpa kila hitaji, chakula nauli na matumizi kwa ajili yake binafsi.
Mawasiliano yetu yalikuwa mazuri na siwezi ongea jinsi alivyonibamba na suprize za kusafiri kwa gari mpaka kuja pale Ilula na kama haitoshi nami nilivyontembelea mara kwa mara na kufurahia maisha yale nikimpa moyo kuwa sasa baada ya yeye kurudi maisha yangebadilika kwa kuwa na mama watoto msomi.
Mida ikayoyoma hatimaye miaka na Antonia akahitimu chuo na kuwa binti wa kwanza katika darasa lile, pale kijijini na hata katika maisha yangu kupata degree.
Siwezi kusema nilifurahije ila nakumbuka mbuzi watatu waliangushwa kwa furaha na kila mtu pale kijijini akasema "Ama kweli mapenzi yana nguvu ya kuihamisha milima kama yakikutana na wenye imani zao"
Kipindi hicho nami nilishajua kuwa kuna kitu kinaitwa masters na alipohitajika kufanya kazi kama meneja wa saccos ya wafanyabiashara pale kijijini nilimkatalia na kumwomba aendele kusoma na kuwa na masters kwani kwa muda huo uwezo wa kifedha nilikuwa nao.
Akakubaliana nami kwa furaha na kusema hilo pia lilikuwa jambo jema kwake na akarudi tena pale akibobea katika fani ya biashara nami nikizidi kujikita katika fani ya kilimo cha vitunguu.
Kuna kitu mara hii kilianza kunitatiza kwani miezi sita baada ya akufika pale, akaanza kuwa mtu wa kutopatikana hewani na akipatikana anakuja na kila sababu mara simu mbovu namwingizia hela anunue mara hiki mara kile.
Nikahisi labda simpi matumizi ya kutosha, ikanibidi niongeze fedha na kumwekea mara tatu ya ile ya mwanzo lakini sasa akaona azime na simu kabisa.
Kipendacho roho hununu bando ili kumsaka fb au whatsapp. Kijana nikaamua kwenda Dar kwa surprize baada kutowasiliana kwa zaidi ya miezi mitatu.
Kufika kile chumba nikaambiwa hajaonekana pale zaidi ya mwezi nikapanda mpaka chuoni kwa rafiki yake aitwaye Chuna nae akanambia hajawasiliana nae ila akanipa namba mpya na kuniambia mpigie.
Antonia alipatikana kupitia namba hiyo na kuniambia yupo Zanzibar anafanya utafiti na akirudi atanitaarifu. Mmmmh ila nilihisi kabadilika na sikuwa na la kufanya zaidi ya kumkubalia na kurudi ilula kiunyonge.
Zilipita siku na miezi bila kuja na mara ya pili kwenda kule nikaambiwa kuwa amehama na pale nikamtafuta bila mafanikio na kurudi nyumbani kwetu nikiwa na majonzi ingawa kuna rafiki yake aitwaye aitwaye Mary yeye alinipasulia kwa kusema kuwa antonia anatembea na mwalimu moja pale chuoni.
Nakumbuka mwanzo niliumwa sana na kuhuzunika kabla ya Fuledi kunipa ushauri juu ya kuwa mvunilivu huku nikitafuta njia muafaka kama yeye atakavyo-deal na michapio anae mwibia post zake lakini bado havikunisaidia.
Miezi mara mwaka ukapita na nikasahau na kuendelea na kazi zangu vyema.
Nakumbuka siku moja nikiwa nimechoka na nimetoka kazini tumekaa tunaangalia filamu mimi na kaka yangu, nikashtushwa na sauti ya muungurumo wa gari na hatimaye mtu akagonga mlango.
Nilipo mkaribisha wakaingia Antonia akiwa na pande la baba limevalia suruali tumboni na baada ya kukaa yule baba kaanza kuongea,
"Mimi naitwa Mr. Salva na ni mkufunzi wa huyu binti ambaye sasa ni mpenzi wangu na awali alikuwa mpenzi wako. Kwa kuwa ameniambia juu ya uhusiano wako na yeye na kuwa ulimsomesha basi nimekuja tuongee kiume ili mimi nikurudishie gharama na unipe baraka za kuoana nae"
Nilitulia safari hii kama nimemwagiwa maji ya baridi nasubiri kumjibu mtu kwa hasira lakini kuna kitu kikaniambia tulia wewe.
Nikamwabia hivi unaweza kunilipa muda, nguvu, mapenzi, uvumilivu na kila kitu nilochowahi mtolea huyu unaemwita mkeo**??????????
Akasisitiza nataka tuishi kwa amani, baada ya mabishano ya hapa na pale kaka yangu mropokaji aitwaye Comfrey yeye akasema tulipeni milioni 30.
Yuke baba akasema haya hamna shida, akauchukua mkoba wake ambao kwa muda huo ulishikwa kipenzi changu Antonia iyekuwa kwa muda huo akijifanya kuangalia chini wakaandika cheki ya shillingi milioni 30 na wakaondoka.
Sikutaka kuzitumia zile hela nikaona kuwa ni laana ila kaka yeye akaomba afanyie biashara nikampa na miezi saba baadae nikaja pata habari kuwa Antonia alimwagiwa maji ya moto usoni baada ya kuja kukutwa na mke halali wa yule baba aliyejifanya hana mke wa familia.
Hadi sasa kaka yangu na mimi tuna biashara nzuri na Antonia uso wake hautamaniki tena na amerudi hapa kijijini hana cha kufanya kwa hofu ya kukaa mjini atachekww na hatamaniki usoni mwake kumtizama zaidi ya mara 2 ila bado anajifanya kunipenda.
Habari hii haina ukweli wowote
Facebook ilivyonikosesha raha 11
Ilikoishia jana
Nilipofika sebuleni hata kabla sijafanya lolote kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya mke wangu na ukanifanya niishiwe nguvu kabisa kwani simu nilikuwa nayo.
Ujumbe huo ulisema...........................................................
Endelea
Ujumbe huo ulisema, " My dear ule muda ndio huu sasa amka na hakikisha hakuoni baba segito na fanya kama nilivyokuelekeza"
Ujumbe huu ulinichanganya zaidi na kunifanya nitoke nje bila kujua wapi nilitaka kuelekea. Nikajiuliza, je hii ni meseji kutoka kwa nani na anataka kumpeleka wapi mke wangu usiku huu?
Nilikaa pale sebuleni kwa muda mrefu sana huku nikiwaza na kujipa majibu ambayo hata hivyo sikuridhishwa nayo na kusubiri kukuche niende kumcheki mama segito.
Asubuhi nikiwa njiani niliijaribu ile namba huku nikihofia kusikia mambo ya ajabu lakini namba ile haikuwa hewani na hata nilipojaribu kuiangalia kama imesajiliwa haikuwa imesajiliwa.
Nilifika pale hospitali kwa kuchelewa kidogo na moja kwa moja nikaingia chumba alicholazwa mke wangu mama segito.
Nilipatwa na mshangao pale mke wangu aliponiona na kukimbilia kwa daktari wa zamu aliyekuwa pale huku akiniita eti mimi freemason nataka kumuua.
Kiuweli nilishikwa na butwaa kwani sikuruhusiwa tena kuingia mle na daktari akaniahakikishia itakuwa ni mshtuko wa jana yake hivyo bado anahofu na hajitambui.
Wakati natoka pale ili nirudi nyumbani pale mlangoni nikapishana na shemeji yangu ambaye ni kaka wa mke wangu na baada ya kusalimiana nae nikaona nimwache aingie peke yake kwenda kumcheki dada yae na mimi nipitie sehemu nipate angalau kifungua kinywa.
Nilikaa pale kwa zaidi ya saa moja na kwenda nyumbani na nilipofika pale nikashangaa baada ya kuonana na binti wa kazi akiwa peke yake bila mwanangu segito na kuniambia shangazi yake ambaye ni mke wa kaka wa mama segito kaja kumchukua.
Wakati nikiendelea kushangaa hayo mara simu yangu ikapigwa...................................................endelea kwa kufuata link hii
http://karibumbeya.com/ads/facebook-ilivyonikosesha-raha-11/

0 comments: