Habari ya kusikitisha!!!! Mama wa ajabu aliyempenda mwanae hata baada ya kufa
Mama mmoja alilazwa hospitali akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa maumivu makali kichwani na alikuwa katika hali mbaya sana.Mwanae wa pekee pamoja na baadhi ya ndugu walikizunguka kitanda cha mama wakijitahidi kumpa msaada wa karibu wakishirikiana na wauguzi.
Muda mchache baadae yule mama akafa kwa kuzidiwa na homa na mwanae alilia sana kiasi cha kukosa nguvu huku ndugu wakimsaidia.
Siku ya pili kijana yule akarudi nyumbani na kufungua kabati la mama yake ili apange vitu vizuri na kuona kuna dawa zimewekwa na barua pembeni yake.
Ile barua iliandikwa, " Chuukua hizi dawa mwanangu kipenzi na uzinywe, najua mwili wako utakuwa na baridi na homa baada ya kunililia sana"
Mapenzi ya mama ni mapenzi ya kweli kwetu sisi hata kama hatuko nao.
Funzo
Hakuna mtu anayeweza kuziba nafasi ya mama katika mioyo yetu
Facebook ilivyonikosesha raha 11
Ilikoishia jana
Nilipofika sebuleni hata kabla sijafanya lolote kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya mke wangu na ukanifanya niishiwe nguvu kabisa kwani simu nilikuwa nayo.
Ujumbe huo ulisema...........................................................
Endelea
Ujumbe huo ulisema, " My dear ule muda ndio huu sasa amka na hakikisha hakuoni baba segito na fanya kama nilivyokuelekeza"
Ujumbe huu ulinichanganya zaidi na kunifanya nitoke nje bila kujua wapi nilitaka kuelekea. Nikajiuliza, je hii ni meseji kutoka kwa nani na anataka kumpeleka wapi mke wangu usiku huu?
Nilikaa pale sebuleni kwa muda mrefu sana huku nikiwaza na kujipa majibu ambayo hata hivyo sikuridhishwa nayo na kusubiri kukuche niende kumcheki mama segito.
Asubuhi nikiwa njiani niliijaribu ile namba huku nikihofia kusikia mambo ya ajabu lakini namba ile haikuwa hewani na hata nilipojaribu kuiangalia kama imesajiliwa haikuwa imesajiliwa.
Nilifika pale hospitali kwa kuchelewa kidogo na moja kwa moja nikaingia chumba alicholazwa mke wangu mama segito.
Nilipatwa na mshangao pale mke wangu aliponiona na kukimbilia kwa daktari wa zamu aliyekuwa pale huku akiniita eti mimi freemason nataka kumuua.
Kiuweli nilishikwa na butwaa kwani sikuruhusiwa tena kuingia mle na daktari akaniahakikishia itakuwa ni mshtuko wa jana yake hivyo bado anahofu na hajitambui.
Wakati natoka pale ili nirudi nyumbani pale mlangoni nikapishana na shemeji yangu ambaye ni kaka wa mke wangu na baada ya kusalimiana nae nikaona nimwache aingie peke yake kwenda kumcheki dada yae na mimi nipitie sehemu nipate angalau kifungua kinywa.
Nilikaa pale kwa zaidi ya saa moja na kwenda nyumbani na nilipofika pale nikashangaa baada ya kuonana na binti wa kazi akiwa peke yake bila mwanangu segito na kuniambia shangazi yake ambaye ni mke wa kaka wa mama segito kaja kumchukua.
Wakati nikiendelea kushangaa hayo mara simu yangu ikapigwa...................................................endelea kwa kufuata link hii
http://karibumbeya.com/ads/facebook-ilivyonikosesha-raha-11/

0 comments: