Fuledi akasema “Baba, Angalia miti inarudi nyuma!”

13:17:00 Unknown 0 Comments





Fuledi akiwa na mika 26 alisafiri kwa kutumia treni akiwa na baba yake, Fuledi akawa akiangalia nje kupitia dirisha la treni na kisha akamwita baba yake kwa sauti kubwa......


“Baba, Angalia miti inarudi nyuma!”


Baba alitabasamu na kuna mtu na mpenzi wake walimwangalia fuledi na kutabasamu kwa ajili ya maswali yake ya kitoto huku umri wake ukionekana kwenda, Fuledi hakujali akamwita baba tena.....


“Baba, Angalia na mawingu yanakimbia nasi, yanatufuata!”

Wale wapenzi walishindwa kuvumillia na kumwambia mzee......

“Kwanini mzee usimpeleke mwanao kwa daktari mzuri?...Maana inaonekana sio mzima”

Mzee alitabasamu na kusema…


“Nilifanya hivyo na tunatoka hospital leo, alikuwa kipofu tangu azaliwe na leo ndio kaweza kuona kwa mara ya kwanza....”
.
.
.
.
Funzo……….
.
Kila mtu katika dunia hii ana hadithi yake tofauti ya kutusimulia......Usiwahukumu watu mpaka uwafahamu vizuri. Ukipata ukweli juu yao unaweza umia na kujiona ulikuwa hakimu mbaya.


Nice weekend ooooooh hey.

You Might Also Like

0 comments: