Gazeti lazua balaaa

13:16:00 Unknown 0 Comments

Fuledi alikuwa akisoma gazeti lake na  wakati huo huo mtoto wake alikuwa akimsumbua kila mara na kumfanya ashindwe kutuliza akili yake kkatika  gazeti lake.

Ili kumfanya mtoto awe bize Fuledi akalichukua gazeti na kulichana sehemu yenye ramani katika vipande vipande ili mtoto aunganishe upya.

Fuledi alikuwa na imani kuwa mtoto Yule angeitumia siku nzima kuunganisha ramani ilewakati yeye akipata nafasi ya kukaa vyema na kumaliza kulisoma gazeti lake bila kuwa na usumbufu wa aina yoyote ile.

Lakini mtoto Yule ndani ya dakika chache alikuja akiwa kaiunganisha ramani ile kwa urahisi kabisa  …….Fuledi alipomuuliza mbona umetumia muda mchache hivi?  Mtoto alijibu,

“Oh….Baba,  kulikuwa na picha ya sura ya mtu upande wa pili wa ramani katika  gazeti……Nikaipanga upya sura  ile na kugeuza upande wa pili ramani ikawa imekaa vyema.”

Mtoto akakimbia nje na kuendelea  kucheza na wenzake huku  akimwacha Fuledi akiwa katika 
mshangao.

Funzo:

Kumbuka kuna upande wa pili wa furaha katika kila jaribu gumu unalolipitia katika dunia hii. Na utapatwa na mshangao kuona jinsi ilivyorahisi kutatua tatizo lako linalokusibu sasa..

Jambo la msingi ni kuwa na matumaini katika mafanikio

You Might Also Like

0 comments: