JINSI YA KUISHI NA MWANAMKE MWENYE HASIRA

12:01:00 Unknown 0 Comments



1 Tafuta sababu ya yeye kukasirika. Angalia hiyo hasira yake imesababishwa na nini. Labda ni wewe ndiyo umesababisha kutokana na kukosekana na maelewano mazuri baina ya kitu anachohitaji na unachohitaji wewe kifanyike. Kaa naye na zungumza naye kwa upole si hasira kwa hasira italeta hali mbaya baina yenu. 

2 Omba msamaha bila kujali nafasi yako ya uanaume. Kama umekosea usikatae kosa muombe msamaha nakiri kosa lako kuwa hutarudia tena. Usimfanye akapandisha hasira zaidi na kuongea visivyofaa mkafika mahali ambapo hutaweza kuhimili.

3. Kuwa mpole katika kipindi ambacho unamuona kuwa mpenzi wako amekasirika. Kwa sababu akiongea na wewe ukaongea kwa hasira hakutatokea maelewano bali makwaruzano zaidi

4. Mtumie ujumbe wa mapenzi zaidi ya zile jumbe alizozowea kuzipata kutoka kwako. Msifie mara kwa mara na ajisikie vizuri pale ambapo ana maumivu ndani ya moyo wake.

5. Mtanie tanie utani wa kumrudisha katika hali ya kawaida ili ajisikie afadhali na kupunguza hasira zake.

... Mada yeyote tutumie inbox tutaijadili pamoja ...

Share and hit like if u ove it


55 people reached
Facebook ilivyonikosesha raha 10

Ilikoishia jana

Nilimkuta mama segito akiwa kapika chakula na ananisubiri ili tule pamoja. kwa uchovu nikakaa kwenye kochi na kumwomba nisile muda huo jambo lililomshangaza sana mama segito.
... See More
Photo: Facebook ilivyonikosesha raha 10

Ilikoishia jana

Nilimkuta mama segito akiwa kapika chakula na ananisubiri ili tule pamoja. kwa uchovu nikakaa kwenye kochi na kumwomba nisile muda huo jambo lililomshangaza sana mama segito.

Ulipita muda wote tukiwa kimya na kisha nikaona nivunje ukimya na kumwambia, " mama segito mke wangu, naomba nik..................................................

Endelea

Ulipita muda wote tukiwa kimya na kisha nikaona nivunje ukimya na kumwambia, " mama segito mke wangu, naomba nikuulize jambo ambalo kiukweli limenishangaza sana siku ya leo hapa nyumbani'

"niulize tuu mme wangu baba segito"

"Naomba unifuate mpaka chumbani" nilinyanyuka na kumshika mkono mpaka chumbani na kulifunua godoro.

Baada ya mke kuona sanda ile alishtuka na kuanguka chini, nilijaribu kumdaka ila nikashindwa na nilipomsogelea pale chini nikaona alikuwa akihema kwa taabu.

Nikamnyanyua na moja kwa moja nikampigia simu ally ambaye alikuja na muda mfupi baadae tulifika katika zahanati moja iliyokuwa nje kidogo ya jiji la mbeya.

Daktari akaniita na kuniambia kuwa mke wangu kaptwa na mshtuko mkubwa sana na kama haitoshi hataruhusiwa ili apate uangalizi wa karibu sana na apumzike.

Niliondoka na Ally na muda huo ilikuwa mida ya saa nne kasoro za usiku hivyo nikafanikiwa kuondoka pale na kwenda moja kwa moja mpaka bar moja maarufu na kuanza kupata moja nikiwa na ally ambaye yeye hutumia sana vinywaji baridi.

Tulikaa pale na nakumbuka mida kama ya saa saba kasoro ally alinipeleka mpaka nyumbani na kuniacha pale. Nilimkuta dada wa kazi ameshanisaidia kumlaza segito hivyo mimi nikapitiliza mpaka chumbani.

Usingizi haukupatikana hivyo nikaona niichukue laptop yangu na kuanza kuperuzi mtandao. Huwezi amini ile nafungua tuu nikaona coletha yuko online na post yake moja imeandikwa " Mchezo ndio unaanza"

Nikashtuka sana na moja kwa moja nikaenda mpaka kwenye block na kumtoa kabisa na nikaifunga laptop yangu na kwenda sebuleni ili niangalie filamu na kuendelea kupata kinywaji kwani yale maneno "mchezo ndio unaanza" alinipa hofu.

Nilipofika sebuleni hata kabla sijafanya lolote kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya mke wangu na ukanifanya niishiwe nguvu kabisa kwani simu nilikuwa nayo.

Ujumbe huo ulisema...........................................................

Nitaendelea kesho mida kama hiii, unaruhusiwa kutembelea www.karibumbeya.com kwani ndio mdhamini wangu

Soma visa vya awali http://karibumbeya.com/ad-category/stories/
343 people reached

You Might Also Like

0 comments: