HAYA MAPENZI MHHH....YAANI ZAIDI YA KIZUNGUZUNGU
[Demu] ana-beep,mshikaji wake kapiga
[demu ](kalegeza sauti):hello baby,uko wapi?
[boy:] niko hapa mwenge,kuna mambo yanilileta huku
[demu:]hivi unajua kama mm naumwa?
[boy:]unaumwa nini?
[demu:]tumbo linaniuma,kichwa nacho sasa ndo basi,yaani kimekuwa kizito kama nimebeba gunia la mahindi, sijui ni kitu gani? kula siwezi,yaani sina hamu kabisa,
[boy:]okay,pole kawaida labda ndo unainagia kwenye siku zako
[demu:] hapana kabisa,hii ni too much,njoo nikuone labda ntapona
boy:]sasa mm niko huku mbali,labda baada ya masaa matatu hivi
[demu:] ww hunipendi najua,yaani naumwa sina hamu ya kula afu unasema unakuja baada ya masaa matatu? kama umenchoka nambie
[boy:]okay,nakuja sasa hivi,napanda gari
demu(kafurahi):kabla hujapanda gari,hapo Mwenge stendi kwenye njia ya kutoa magari,kuna ka-supermarket,ingia humo afu nunua maziwa ya unga Nido lile kopo kubwa,humo humo wanauzaga na juice,nunua kopo mbili,moja ya embe nyingine ya apple,mwambie muuzaji akupe na pakiti kubwa ya soseji basi afu ukitoka tu hapo kuna jamaa wana mkokoteni wanauza matunda,nchukulie parachichi,nanasi hata ndizi pia! nataka nione kama ntarudisha appetite.
[boy:]umemaliza?
demu ndio,basi wahi mwenzio nina hali mbaya hujui tu,afu niletee na vocha mwenzio nina deni kwenye line yangu.
[boy:]umesahau mzani,na calculator
[demu:] hayo ya nini? na ww kwa utani hujambo
[boy:] maake naona unataka kufungua supermarket nyingine huko kwenu. Sasa nsikilize ww mende,siji kama unaumwa hadi unapelekwa ICU haya wasalimie,yaani sijawahi ona mtu anakula kama ww afu unajiita mgonjwa! Fala ww,mbona sijasikia ukisema unataka dawa?,usinipigie simu,kamweleze baba yako hayo mambo
0 comments: