KISA CHA KWELI KILICHOMFANYA BINTI WA FACEBOOK AANGUSHE MACHOZI BAADA YA KUSOMA JINSI JAMAA ALIVYOPITIA MAKUBWA

20:30:00 Unknown 0 Comments




Nilifika asubuhi pale ofisini na kuhisi hali haikuwa kama kawaida yetu kwani kila mmoja alikuwa kanuna na wengine hata hawajibu salamu zangu.

Nikashangaa sana ila nikajipa matumaini kuwa labda ni jumatatu kila mtu kaamka na stress zake hivyo nikaachana na kuelekea kwenye meza yangu.

Haikupita hata dakika akaja Abdalah ambaye kwa kipindi hicho alikuwa msaidizi wangu na kuniambia kuwa muda huo nilihitajika ofisi kuu.
Wakati nasimama kuelekea ofisi kuu alicheka kwa dhihaka na baadhi ya wafanyakazi wenzangu wakacheka pia.

Niliumia na kujikaza kwani nilishajua mchezo mzima na hasa nilipovujishiwa na secretary wa ofisi kuwa walitamani sana kina Abdalah kuona mimi naachia ngazi.

Wakati najiandaa kuugonga mlango wa mkuu nikawa  najua kuwa lazima itakuwa ni wito wa mpango mpya wa kazi na wiki hiyo nilitakiwa kusafiri .
Niliingia na kumkuta boss upara kama wengi tulivyozea kumwita akiwa kakaa na kikombe chake cha kahawa na kabla ya kuongea kuna mgeni mmoja aliingia moja kwa moja bila kubisha hodi.

Ujio ule ukamfanya meneja anipe barua na kuniambia nikaisome kisha ataniita. Nianyanyuka na kuufuata mlango kuelekea ofisini mwangu.
Nikakuta kuna kikombe cha kahawa mezani nikakinyanyua na kabla sijainywa ili nisome nini kilichoko kwenye barua, yule secretary alikuja haraka na kunipa ishara ya mimi kutoinywa ile kahawa ikifuatiwa na sms.
Nikajivuta pembeni na kuisoma ile sms ambayo iliandikwa, " chai hiyo inasumu" 

Sikutaka kuamini lakini huku barua yangu iliwa mfukoni, nikaondoka mbio mpaka nje nikiwa na kikombe kile na kumwagia kwenye nyasi fulani ambazo mbele yake kuna mbuzi alikuwa akizila.

Mbuzi yule alisogelea pale na kula zile nyasi na hazikupita dakika hata tatu akanza kutokwa na povu mdomoni na muda mchache akafa.
Nikarudi mpaka ofisini kwangu sikutaka kumwambia secretary asante ili wasije gundua kama ameniambia kwani nilihisi waliofanya mchezo huwa walikuwa wakifuatilia hali yangu kwa wakati huo.

Sikutaka kufikiria suala la kahawa kwa wakati huo na ni nani aliyeniwekea hiyo simu ila sasa nikaichukua ile barua kuona meneja kaandika nini.
Hata kabla sijasoma meneja aliniita na kwenda tena ofisi yake bila hata kuisoma ile barua. Nilipoingia wakati huu alikaa kwa masikitiko na kuniambia.

Dan kama ulivyosoma kwenye barua nami sina jinsi kwani ni maamuzi ya kutoka huko juu na wajua mimi ni sawa na mbwa asiye na meno nimeambiwa nikupe na kukuambia kuwa ofisi haiitaji tena huduma yako.

Hivyo utamaliza taratibu za kiofisi na kukabidhi ofisi na pia suala la mkopo uliochukua amedai kuwa atashikilia malipo yako ya akiba yako na nafikiri hutochukua kitu kwani hata hivyo utatakiwa kuongeza fedha kidogo ili uwe umetimiza malipo yote.

Nikakumbuka kuwa nilikuwa nadaiwa pale ofisini fedha nyingi ambazo nyingi nilizitumia kumuguza mzazi na mambo fulani nyeti.

Nikanyanyuka na kwenda ofisini kwangu na kuanza taratibu za kukabidhi ofisi lakini muda huu sikuumia kuhusu kazi wala maisha ya hapo ila jinsi nilivyoweza kuokoka kifo.

Nilikamilisha utaratibu na kuelekea nyumbani ambako nilikutana na mke wangu akiwa katika wheel chair ambacho amekuwa akikitumia kwa kwa miezi tisa sasa tangu apate ajali ya daladala na kupata ulemavu wa miguu.

Nikambusu na kuongoza ndani ambako nililala kwa muda kabla ya kuamshwa na kilio cha chini chini kutoka kwa mke wangu. Nikamfuata na ili nijue nini kulikuwa kikimsibu.

Alikuwa kashika simu na kunionesha ujumbe ulimo ndani yake ambao uliandikwa, " mmeo kafariki asubuhi hii"

Kuangalia muda ambao ujumbe huo ulitumwa ilikuwa asubuhi mida ya ile kahawa. Nikamuliza yeye ameiona muda gani? 

Akaniambia ameiona nilipiingia tu na akawa na hofu kwa nini nimepitiliza kulala au naumwa au nimekula kitu kibaya maana sio kawaida yangu.
Nikamtoa hofu na kuingia jikoni kuanza kumwandalia chakula huku nikisubiri muda muaka ufike nimwambie juu ya mkasa wangu.

Nusu saa baadae watoto walirudi kutoka shuleni na tukajumuika kwa chakula cha mchana ikifuatia na story ya yaliyonisibu.

Alilia sana mke wangu na kuona kama mwaka ule ulikuwa ni wa laana kwetu ila nikampa moyo kuwa tutasonga na yeye atapona na kunisaidia kusaka kupato.

Kiukweli maisha yalibadilika ndani ya muda mfupi hali ikawa ngumu sana pale nyumbani.

Ilifikia kipindi watoto wakatakiwa kuondoshwa shule na ada ya shule ikawa taabu kupatikana na pamoja na kuwa baba yangu alikuwa na fedha sana katu sikutaka anisaidie.

Nilikumbuka jinsi alivyonitimua miaka mitano iliyopita nyumbani kwake tena usiku wa manane huku nikiwa na majereha baada ya kupigwa na kundi la wahuni ambao inasemekana waliandaliwa na wafanyakazi wa kampuni ya baba niloyokuwa nikiisimamia kama mwana wa pekee wa mzee yule kwa mke wa kwanza.... Nikaishia kulia.

Nikaangalia jinsi nilivyojitahidi kumpa ushirikiano na wanae kwa bibi mdogo wakitumbua mali na kuishi maisha ya anasa huku kesi zao zile nikibambikizwa mimi, nikaona sina haja ya kumwita baba nikainuka na kukumbuka nipo mbali ambako asingeweza kujua nikiwa na maisha yangu na niwapendao.

Nikainuka na kujiangalia kwenye kioo nakuon nguvu, uvumilivu, ubunifu na kila aina ya ujasiri machoni mwangu nikamgeukiwa mke wangu na kumwambi hakika huu sasa utaenda kuwa mwaka wa ushindi.
Ishatimu saa kumi na mbili za asubuhi, nikaingia chumbani kwa watoto kuwaamsha wajiandae kwenda shule.

Binti yangu ambaye ni wapili kuzaliwa akaamka na kuufungua mkango aende nje kumwangalia mbwa wake aliyekuwa akimpenda sana na mimi nikamchukua kaka yake kwenda kumwogesha
.
Nikiwa bafuni nikashtushwa na sauti ya binti akiniita nikaelekea kule, sikuamini kuona kwani pale mlangoni kulikuwa na bahasha kubwa ya kaki na ndani yake kulikiwa na fedha.

Nikaogopa kuzichukua na kumuuliza mtoto kama alizishika akakataa nikaingia ndani bila kuzigusa na kumwambia mke wangu na kisha kumchukua na kiti chake mpaka pale na kunishauri nisiziguse.

Niliziacha na kwenda kuwapekeleka watoto ingawa nilijua hakuna ambaye angeingia pale ila nikahisi labda ni wafanyakazi wa ofisini sasa wanataka kuniletea fedha za kichawi nife kwa kuwa wamejua sina hela au kuna mchezo mchafu.

Masaa mawili baadae nikarudi baada ya kuwapitia jamaa zangu na kupata mpya kuhusu kazi kwani nilishakaa zaidi ya miezi kadhaa nikiwa sina kazi kisha nikarudi nyumbani.

Nikazikuta zile hela na wakati huu nikapiga moyo konde bila kumshirikisha mke wangu nakusema kuwa nazichukua na kama kufa nife mtu gani atanitegea nyumbani.

Nikazichukua na kuingia nyumbani na kupitiliza bafuni nikazihesabu zilikuwa ni milioni tatu laki moja na nusu fedha kamili ya ada nilizokuwa nikidaiwa za kodi ya nyumba kwa zaidi ya miezi 9.

Nikaona nisilipe fedha ya nyumba kwani baba hakuwa mkali na kwenda kulipa fedha ya ada ya watoto.

Nilipofika shuleni nikashangaa baada ya mhasibu kuniambia kuna mtu alienda jana yake kulipa. Kwa hofu nikamwomba kuwa watoto wasitoke shule wakiwa wenyewe nitakuwa nikiwafuata na sio basi tena nikihofia huyo mlipaji kuwa alikuwa na njama na wanangu.

Nikapitia benki na kuziweka fedha zile nikiwa na wasiwasi na kumfuata mke wangu nyumbani. 

Alishangaa kwa nini nilichukua zile fedha na  kuna mtu gani kalipa zile fedha shuleni kwa watoto?

Tulikaa kwa hofu bila mtu kujitokeza na nikatumia zile fedha kusajili kampuni binafsi ili niweze kukidhi mahitaji ya nyumbani na kujiajiri pia.
Nilianza kwa shida na wakati huu yule secretary wangu aliyeniokoa kwa kifo cha sumu nilikuwa nikifanya nae kazi nikiwa nimemwajiri.

Maajabu yakawa kwamba kila nikiwa na nyakati ngumu ya fedha za ofisi pango la nyumba au ada za wanafunzi basi nikaamka na kuona pale nje kuna ile bahasha ya fedha.

Siku moja nikiwa ofisini na mke wangu baada ya yeye kupona na nikiwa nasaidiana naye kazi kama mhasibu nilipokea email moja kutoka katika shirika moja wakinitaka nionane nao na wanataka kunifadhili katika moja ya mawazo yangu waliyoyapenda.

Nilionana nao na kweli wakanipa ufadhili mkubwa sana na kunisimamia kwa miezi sita na wakaniomba nijiandae kukutana na boss wa ufadhili huo kwani baada ya kunikagua angeidhinisha malipo zaidi kwa miradi yangu mingi.

Nikakubali na miezi minne baadae nikaambiwa atakuja nami nikaandaa mapokezi na hatimaye siku ilafika.

Siku ilipofika niliumia na kushtushwa kuona ni baba yangu ambaye ndio mfadhili wangu na mbaya zaidi ndio mhusika wa mimi kupigwa na wale wahuni katika kampuni yake, kufanyiwa jaribio la kuwekewa sumu na lile la kufukuzwa kazi na hata mlipaji wa  zile fedha na ufadhili pia.


Nilimuuliza kwa nini uliamua kunifanyia hivyo?

Majibu yake yakawa hivi:-

1. Wakati uko kwenye kampuni yangu pamoja na kujituma ila hukuthamini maslahi ya wadogo ( nikakumbuka ni kweli )

2.) Ulivyoambiwa kuwa umewekewa sumu hukumchukia mtu zaidi ulianza maisha mapya ( nikakuna kichwa)

3. Ulipokosa fedha pamoja na mkeo kuwa mlemavu kwa kipindi hicho mapenzi yako yalizidi (nikatabasamu)

4. Ipopata fedha usizozijua ulikuwa mwangalifu na kuwa na kampuni ( nikashangaa)

5. Pamoja na yote ukamkumbuka aliyekuokoa na kuwa secretary wako pia ( ikanipa nguvu)

6. Mkeo ukamashirikisha kwenye kazi zako.... Nikafurahi hapa.

7. Maisha yalipokuwa magumu ukapanua uwezo wako wa kufanya kazi kwa ufasaha na sasa nafurahi kuwa na mpiganaji na kumbuka ni mpango wa baba kumfanya mwanae kuwa shupavu na jasiri
Kuna kitu twajifunza hapa

You Might Also Like

0 comments: