Kwa nini nawachukia baadhi ya wanaume
Kuna wakati ni vyema kutambua kuwa hawa mabinti ni dada zetu, shangazi zetu, mama wadogo, binamu na hata shemeji zetu watarajiwa.
Unakuta mwanaume anamfuatilia binti kwa mbwembwe nyingi kila post hapa facebook atamtaja huko mtaani ndio usiseme kila mahali atajitahidi kuwa na binti na kuziteka hisia za binti.
Miezi michache baada ya kutanua miguu ya binti wa watu na kumchakaza mwenzie mara binti anajikuta ni mjamzito na kumwambia jamaaa jamaa anaanza kukwepa majukumu na kumwacha mtoto wa watu akiwa anahaha jinsi ya kuieleza familia yake huku baadhi ya ndoto zikipotea kwa muda ili akabilaiane na suala hili.
wakati huo jamaa kaanza kupaisha fb binti mwingine na siajabu akarudia mtindo huo huo.
Hebu tufikiri pamoja
Vipi huyo anayefanyiwa hivyo angekuwa mdogo wako au hata binti unayetajaria kuishi nae?
Vipi nawe ungechezewa feeling na mwisho kuishia mchezo huo?
Nasema hivyo kuna binti mmoja jana aliniita na kunialika kwake na kunisimulia jinsi maisha yake yalivyoharibiwa na kijana mmoja na sasa dada amelazimika kuihama familia kisa wanamwona kama ni malaya asiyetakiwa kuishi nao kwani wao wameokoka.
Na kwa udadisi wangu inaonekana jamaa alitumia ushawishi mkubwa na kumrubuni binti mpaka ikawa hivi.
Kwa wale wanaume wa tabia hii........ Guys hebu tuwe na huruma ni mara mia utumie hata kinga ukijua dhamira yako ni feki ili mwezie safari na ndto zake zisikatishwe tumhukumu kwa kutokushinda vishawishi na sio kumwacha mtu na mzigo wako na huwezi kumsaidia matunzo....
NINA HASIRA
nawe kama una hasira like Tabasamu na Fuledi kisha share tuokoe dada zetu
0 comments: